CHAMA CHA CUF CHAMBANA RAIS MAGUFULI NA SERIKALI YAKE,NI KUHUSU ZOEZI LA BOMOA BOMOA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Magdalena Sakaya akizungumza na wanahabari hawapo pichani |
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeitaka serikali ya Rais John Magufuli kuacha kutumia
ubabe kwa kuendelea zoezi la bomoa bomoa kwa Wananchi, kwa madai zoezi hilo
linakasoro lukiki ambazo zinakwenda na kinyume na haki za binadamu.Aaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kauli ya
CUF inakuja ikiwa ni siku moja kupita baada ya ofisi ya Makamu wa Rais kuibuka
kutangaza kuhamishia zoezi la BomoaBomoa katika Bonde la mto Msimbazi Jijini
Dar es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo mapema jijini Dar es Salaam,Naibu Katibu mkuu wa CUF
bara,Magdalena Sakaya amesema Chama chake kimefanya utafiti tangu zoezi la
bomoa bomoa lilipoanza na wamebaini zoezi hilo limejaa mapungufu makubwa ambayo
anadai yanamtesa mwananchi.
“CUF
tumefanya uchunguzi na kubaini kwamba kuna kundi kubwa la wananchi wamebomelewa
makazi yao na kuharibiwa sehemu zao za biashara kimakosa”amesema Bi Sakaya.
Mheshimiwa
Sakaya ameyataja makosa hayo ni maeneo ya makazi ya wanaoishi maeneo ya mto
msimbazi akidai kunawakazi wameishi miaka mingi
na wanahati za nyumba, ambapo ameeleza mwaka 2012 walitakiwa kupewa
viwanja maeneo ya mwabepande lakini hawakupewa viwanja hivyo anashangaa kwanini
serikali inawavunjia,
Vilevile
Sakaya ameendelea kuitupia lawama serikali akidai ndio iliyopelekea wananchi
kujenga katika maoneo ambayo anakili ni hatarishi akidai kuwa serikali ilishindwa
kusimamia katiba ya nchi.
“Nchi
yetu inakatiba na sheria na inawasimamazi na wafuatiliaji wa utekelezaji wa
hizo sheria ili kuhakikisha wananchi
hawastahili kujenga maeneo hayo inakuwaje kipindi chote hicho wananchi wajenge nyumba zao wameishi kwa miaka
takribani 2o eti leo unaibuka na kusema wamekiuka sheria,huu ni uzembe wa
serikali”
Hata
hivo,Sakaya ameonesha masikitiko yake kwa Waziri Muungano na Mazingira,Januari
Makamba kwa taarifa yake aliyoitoa jana kwa kusema sehemu ya nyumba
zilizobomolewa ni zile ambazo watu wake wamekwisha amua kubomoa wenyewe.
Akipinga
hoja hiyo,Sakaya amesema Chama cha CUF kimefanya utafiti kimegundua licha ya
nyumba hizo kubomolewa lakini bado wananchi wanaendelea kushia sehemu hiyo
iliyobomolewa huku akishangaa kwa kusema kama walikuwa wanabomoa wenyewe mbona
wapo wanaishi kwenye nyumba walizobomoa.
“Katiba ya nchi sehemu ya tatu kifungu cha 12 na 13
3 suala la haki na utu wa kibinadamu ni serikali haijazingatia hata kidogo zoezi la bomoa bomoa kunavitendo dhahiri vya
kudhalilisha utu na thamani ya utanzania kwa mfano serikali inabomolea nyumba
bila hata kujiridhisha kuwa usalama wa maisha ya watu yanaziingatiwa”ameendelea
kuongeza sakaya.
Pamoja na hayo yote,Sakaya ameitaka serikali ihakiki
inawapatia huduma za kibinadamu wakazi
wote waliobomolewa nyumba zao na hivi sasa ambao amedai hawana makazi ya kuishi
Hakuna maoni
Chapisha Maoni