WAZIRI NYALANDU ACHAFUA HALI YA HEWA,NAYE AZOMEWA BALAA,SOMA HAPO KUJUA
WAZIRI wa
Maliasili na Utalii na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro
Nyalandu amezomewa na wananchi kwenye mdahalo uliofanyika Ukumbi wa parokia ya
Ilongero 11 Oktoba mwaka huu. Anaandika Josephat Isango … (endelea).
Wakizungumza
kwa simu na MwanaHalisi Online kwa simu toka Singida watu waliohudhuria mdahalo
huo unaoratibiwa na Azam Tv katika kipindi chake cha panga pangua, wamesimulia
kwa Nyalandu alizomewa sababu alizungumza uongo.
Kipindi hicho cha
panga pangua ambacho kitarushwa kupitia Azam TV, kiliwakutanisha Lazaro
Nyalandu wa CCM na David Djumbe anayegombea kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendele (Chadema).
Nyalandu alifika
katika kijiji cha Ilongero kwa kutumia helkopta kuhudhuria mdahalo huo uliohusu
sera na ilani za vyama na namna watakavyokabiliana na changamoto za
Miuondombinu, sekta ya maji, umeme n.k.
Ni katika majibu
hayo ambapo Nyalandu alikataa kufuta michango ya shule, na kuanza kukisifu
Chama cha Mapinduzi badala ya kuzungumzia changamoto zinazowakabili wananchi
wake.
Chanzo change , kilipomtafuta Nyalandu hakupokea simu hata baada
ya kuandikiwa ujumbe hakujibu.
Nyalandu
anayegombea Ubunge kwa awamu nyingine anadaiwa kuwa na mahusiano mabaya na
baadhi ya wananchi wa jimbo lake. Ilidaiwa kuwa Aprili 11 mwaka 2012, saa 6:00
usiku katika kijiji cha Mwanyonye, Nyalandu na watu wengine waliotajwa kuwa nao
ni Elia Digha pamoja na Reuben walifika na gari No. T.505 BKM, aina ya VX,
walikuta kizuizi kilichowekwa
na serikali kwa ajili kukagua mazao ya wanyama na misitu, walishuka na
kuwatishia walinzi kwa bastola, wakavunja kizuizi, na kuondoka na taa ambayo
walinzi hao waliitumia. Baada ya tukio hilo Wanakijiji wa Mwanyonye walipiga
simu kijiji kinachofuata.
Kijiji kinachofuata ni Kinyeto, Afisa Mtendaji wa Kata ya
Kinyeto na walinzi walijizatiti ili wazuie ile gari itakapofika, walipofika mtu
mmoja alishuka kwenye gari haraka akiwa amenyoosha bastola na kuwauliza walinzi
mnafungua au hamfungui, walikataliwa, wakavunja kizuizi.
Haijulikani Nyalandu alikuwa anatorosha nini katika mazingira
hayo. Ila walinzi walipopiga picha gari hiyo, na kuchukua namba za usajili,
waliripoti polisi mapema kufungua jalada SI/IR/1570/2012 , Kamanda wa polisi
Mkoa wa Singida hakupatikana kuzungumzia tuhuma hizi zilitatuliwa vipi hadi
sasa.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni