WAISLAM WAITOLEA LAWAMA SERIKALI YA SAUDI ARABIA,NI BAADA YA VIFO VYA MAHUJAJI,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
HUKU kikiwa
bado haijafamahika idadi harisi ya Mahujaji wa kitanzania walifariki nchini
Saudi Arabia,nao viongozi wa dini wa dhehebu la shia nchini wameibuka na kuilahumu serikali ya
nchini Saudi Arabia kwa kupelea vifo hivyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari mda huu Jijini Dar es Salaam,Mwalimu na msomi wa katika
theologia ya Uislam wa umoja wa Mahujaji Shehe Abdulmalik Swaleh ambaye –
naye
alikuwa miongoni mwa mahujaji wa kitanzania waliokwenda kuhiji,ambapo amesema
vifo hivyo vya kusikitisha vya watu wanaofikia elfu nne zimesababishwa na
serikali ya Saudi Arabia kutoweka mazingira mazuri kwa mahujaji hao.
Amesema
hata miundombinu ya barabara katika nchi hiyo zilikuwa ndogo sana ukizingatia
na idadi kubwa ya watu waliokwenda kuhiji,
“Serikali ya
Saudi Arabia inapaswa kupewa lawama,mahujaji tulikuwa wengi sana kuriko hata
miundomini ya barabara iliyokuwepo,watu tulikuwa tunakanyagana harafu hali ya
joto ndio maana hata vifo hivyo”
Viongozi wa Dhehebu ya Shia wakitoa malalamiko kwa serikaliya Saudi Arabia |
Aidha,
Shekh Swalehe ameitupia pia lawama tena serikali ya nchi hiyo,kwa kubadirisha
mfumo mzima uliozoeleka wa kwenda kuhiji,
“Hata mfumo wa kuhiji umebadirika sana,kwani wakati
tunakwenda kutupia jiwe shetani tulikuwa
tunatupa jiwe harafu tunaondokea kwa njia hiyo hiyo,ila sahivi tunashangaa sana
tunakwenda baada ya kutupa jiwe tunarudi njia hiyo hiyo kwahiyo unakuta watu
walikuwa nyuma yetu tunagongana na kuanza kukanyaganya”amesema
Hakuna maoni
Chapisha Maoni