SERIKALI YACHARUKIA PICHA HIZI.NI ZILE ZA TWIGA KUSAFIRISHWA,YAIBUKA NA KUSEMA HAYA,SOMA HAPO KUJUA
WIZARA ya Maliasili na Utalii imesema hakuna Twiga
yeyote aliyetoroshwa toka kwenye mbuga
za wananyama na kupelekwa nje ya nchi katika kipindi hiki.Anaadika KAROLI
VINSENT endelea nayo.
Kauli
hiyo ya wizara inakuja kukiwa na picha mbali mbali zikiwa zimeenezwa kwenye
mitandao ya kijamii zikionyesha uwepo wa Ndege kubwa ndani ya mbuga za wanyama
huku picha hizo zikionyesha watu watano wakiwa wanampakiza Twiga kwenye Ndege kama ambavyo unaziona hapo.
Akitoa
ufafanuzi wa picha hizo,Katibu mkuu wa Wizaya ya Maliasili na Utalii Dk
Adelhelm Meru leo Jijini Dar Es Salaam wakati
wa mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema picha hizo ni za kutengeneza
kwani hakuna mnyama yeyote aliyesafirishwa kwenda nje.
“Watu wamekuwa wanatumia suala hili kisiasa kwa
kupakua picha za internet kutoka nchi zingine wanazitengeneza na kusema za hapa
nchini”amesema Meru
Amesema kuwa “Twiga ni nembo muhimu kwa Taifa
letu,hairusiwi kuwindwa na kusafirishwa mnyama huyo”
Aidha Dk Meru amekiri kuwepo na wageni kutoka nchi
za nje,wanaokuja kuwinda katika mbugu zetu jambo analodai limekuwa likiliingiza
Taifa mapato makubwa.
Amefafanua kuwa katika kipindi hiki mfalme mmoja
kutoka nchi za kiarabu alikuja kufanya uwindaji kwa mda wa siku nne yaani toka
Semptemba 24 hadi 29.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni