JOB NDUGAI AKUNWA NA SERA YA LOWASSA,AMUA KUSEMA YAMOYONI,SOMA HAPO KUJUA
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kogwa kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Job Ndugai akihutubia mkutano wa kampen |
MGOMBEA Ubunge
Jimbo la Kogwa kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Job Ndugai, amesema
iwapo atachaguliwa kuliongoza jimbo hilo kwa awamu ya nne, atahakikisha
anatatua mgogoro kati ya wakulima wa Wilaya ya Kogwa na wafugaji wa wilaya ya
Kiteto mkoani Manyara. Anaandika Pendo Omary … (endelea).
Akizungumza
na Chanzo changu, Ndugai ambaye pia ni Naibu Spika amesema: “Sababu kubwa
iliyopelekea kukua kwa mgogoro huu ni mzaha, ubinafsi na uzembe uliokuwa
ukifanywa na baadhi ya viongozi wa serikali wilayani Kiteto katika kusuruhisha
mgogoro kati ya wafugaji na wakulma.”
“Iwapo nitapewa ridhaa ya kuiongoza
Kogwa kipaumbele cha kwanza ni kurejesha amani kati ya wakulima na wafuagaji
katika wilaya za Kiteto na Kogwa. Tutakaa chini na viongozi ili kutatua tatizo
hili,” amesema Ndugai.
Mbali na Kauli hiyo, Ndugai pia
anakubaliana na kauli ya Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema kupitia mwamvuli
wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa kuhusu kuunda tume ya
maridhiano itakayoshughulika migogoro ya wakulima na wafugaji ili kuondokana na
matatizo ambayo yamekuwa yakiwasumbua, iwapo atachaguliwa kuwa rais wa awamu ya
tano.
Lowassa alitoa kauli hiyo wiki
iliyopita wakati wa mkutano wa kampeni katika uwanja wa Soweto wilayani Kiteto.
“Wazo
alilolitoa Lowassa ni zuri hasa kwa mtu yoyote anayependa amani ipatikane. Ni
aibu Watanzania kuchinjana. Viongozi tutakaochaguliwa kutumikia wananchi ni
lazima tukae chini ili kumaliza tataizo hili. Tunahitaji kuwa na mipango, wala
hatuhitaji kuwa na fedha za kigeni kumaliza migogoro,” amesema Ndugai.
Mwaka
2014 Watanzania walishuhudia mauaji ya kutisha ya watu 10 wilayani Kiteto
katika kile kinachotajwa ni mgogoro baina ya wafuagaji na wakulima ambao
wanahangaika kutumia eneo la ardhi kwa ajili ya mahitaji yao.
habari hii kwa hisani ya mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni