Zinazobamba

CCM NA SERIKALI WALICHARUKIA GAZETI LA MWANANCHI,MWAMBENE WA MAELEZO AIBUKA ASEMA HAYA,SOMA HAPO KUJUA

Pichani ni Mkurugenzi wa Maelezo
Assah Mwambene

NA KAROLI VINSENT
IKIWA imepita siku chache tu baada ya Chama cha Mapinduzi CCM kuwafukuza waandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi kwenye ziara za Kampeni za mgombea wa Urais kupitia chama John Magufuli kwa madai ya kuandika habari tofauti na matakwa ya chama hicho.
Nayo pia Serikali ni kama imevilivaa Gazeti hilo kwa kusema limeandika habari ya uchochezi na uongo ambazo zimeleta msuguani kwa jamii.
 Kwa mujibu  wa taarifa iliyotolewa na  Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo ,Assah Mwambene kwenye vyombo vya Habari imesema tahariri ya gazeti la Mwananchi,toleo Na.5545 la tarehe 30 semptemba,yenye kichwa cha Habari kisemacho  “Rushwa inazidi kutudhalilisha mbele ya dunia”
   Mwambene amesema tahariri hiyo imesema uongo wa wazi,inao ukweli nusu na pia imejaa upotoshaji ambao anasema haipashwi kuandika kwa gazeti kubwa kama mwananchi.
Amesema uongo huo umefanywa kwa makusudi ili kuitia doa serikali ya Rais Jakaya Kikwete na kuchafua haiba ya Tanzania mbele kwa jamii na duniani kwa ujumla.
Amefafanua kuwa tahariri ya Mwananchi inasema kuwa Bodi ya  Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Milenia “Millenium Challenge Account” kwamba ilizuia msaada wa dola za kimarekani 4752 kwa Tanzania amesema ni upotoshaji
Amedai kuwa Modi ya MCC,kwenye kikao cha tarehe 17 semptemba mwaka huu,iliipongeza Tanzania kwa kufanya vizuri  kwenye  vigezo vyote vya kustahili msaada kupitia MCC,ambapo katika kikao hicho walitoa kigezo kwa Tanzania  kuhusu rushwa.

  Sanjari na hayo Mwambene amesema Gazeti hilo linavyooilahumu Ubarozi wa Marekani hapo dare s Salaam na serikali ya Tanzania  kuwa ati taarifa  azitozeleshwa,ambapo amedai Mwandishi makini,na mhariri madhubuti,haandiki tahariri ya upotoshaji kama huo.

Hakuna maoni