MAGUFULI AINGIZWA MKENGE DODOMA,SOMA HAPO KUJUA
MGOMBEA urais wa
Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli amedanganywa kuhusu
mwenendo wa mtu aliyejitambulisha kwa viongozi wa CCM kuwa ni kiongozi katika
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na msimamizi wa kampeni ya mgombea
ubunge jimbo la Dodoma mjini. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Zoya alipopandishwa jukwaani siku Dk. Magufuli alipohutubia mkutano
mkubwa wa kampeni Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kwamba yeye ni Katibu Mwenezi
wa Chadema ngazi ya Wilaya na pia msimamizi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo
la Dodoma mjini (Chadema), Benson Kigaila.
Mwandishi wa habari
hizi kwa uchunguzi alioufanya, amethibitisha kuwa Zoya hakuwa na wadhifa huo na
wala hakuwa msimamizi wa kampeni za Kigaila.
Taarifa za uongozi
wa Chadema mkoani zinasema Zoya alikuwa mwanachama wa kawaida ambaye aliwahi
kushika kuwa Katibu Mwenezi ngazi ya Kata ya Chang’ombe.
Imebainika kwamba
Zoya alishindwa kuchukua fomu ya kugombea udiwani, badala yake akagombea
udiwani katika Kata ya Majengo.
Uchunguzi umebaini
zaidi kuwa Zoya amekuwa mtu maarufu wa mwenendo wa kuhamahama hata dini huku walio
karibu yake wakimtaja kama mtu mpenda maslahi binafsi zaidi ya kitu kingine.
Zoya wakati
akijulikana ni Mislamu, ghafla alibadilisha dini na kujiunga na Ulokole ambako
pia aliacha na kurudi kuwa Muislamu; baadaye akatoka tena Uislamu na
kubadilisha dini akawa Msabato anakoendelea kwa sasa.
Hatua yake ya
kujitangaza kwenye mkutano wa CCM kwamba alikuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA
Wilaya ya Dodoma na msimamizi wa kampeni za Kigaila, imesukuma Baraza la Vijana
wa Chadema (BAVICHA).
Mwenyekiti wa
BAVICHA Wilaya ya Dodoma Mjini, Fibert Musa Muhoja ambaye ni Mwenyekiti wa
BAVICHA Wilaya Dodoma Mjini alisema Baraza la vijana Chadema(BAVICHA) Wilaya ya
Dodoma mjini amesema inasikitisha unakuwa na kiongozi anayepotosha umma.
Muhoja amesema
viongozi wa CCM walipo mjini Dodoma wanajua vizuri ukweli huo wa mwenendo wa
Zoya lakini hawakumjulisha Magufuli, jambo ambalo Muhoja anasema viongozi hao
walilifanya kwa nia ya kumzuga mgombea wao kwa maslahi binafsi ya kuonekana
wamemfanyia kampeni ya Magufuli.
“Ukweli mmoja haufutiki
kuhusu mwenendo wa Zoya… ni mtu anayehamahama hata dini inayohusu uhusiano wa
binadamu na Mwenyezi Mungu. Mtu akiwa si muaminifu kwa Mwenyezi Mungu
hashangazi kuwa mbabaishaji kwa binadamu wenzake,” alisema.
“Huyu Zoya tunamjua na hata viongozi wa CCM hapa Dodoma wanamjua
vizuri, ni mkazi wa Chang’o mbe na kazi yake ni fundi cherehani na elimu yake
ni darasa la saba,” amesema.
“Mwaka 2010 Khalid Zoya alinunuliwa na kupoteza Kata ya Majengo
kwa mgombea wa CCM ambaye kwa sasa anatetea nafasi hiyo Msinta Mayauyau.
“Katibu Mkuu wa CCM aliyekuwepo kabla ya Wilson Mukama, Luteni
Yusuph Makamba alimpatia Zoya vyerehani viwili na shilingi laki tatu ambayo pia
walidhulumiana na baada ya muda, Zoya alirudi Chadema,” alieleza Muhoja.
“Pia sisi Baraza la Vijana tumesikitishwa na yeye kujipa vyeo
ambavyo kimsingi hajapata kushika akiwa Chadema. Mpaka sasa tunavyoongea katibu
mwenezi wa Wilaya ya Dodoma Mjini ni Juma Bika Mtaalam, japo alisimamishwa
uongozi kwa muda na ndio amekuwa Kampeni Meneja wa mgombea ubunge jimbo la
Bahi, Mathias Lyamunda,” amesema.
“Suala la yeye kujiita kampeni Meneja wa mgombea ubunge wa jimbo
la Dodoma Mjini ni la uongo na tunaomba wananchi wampuuze maana ni cheo
alichokuwa akikitaka na sisi tunaamua kwa vikao, hakuna muhtasari wa kikao
chochote uliopitisha jina lake kuwa Kampeni Meneja…
“Tunajua amepewa shilingi laki 7 na kuahidiwa kununuliwa
vyerahani vingine viwili, na kupangishiwa fremu ya ofisi ya kushonea,” amesema
Muhoja.
Zoya pia aligombea ukatibu wa Bahi mwaka 2010 akashindwa,
aligombea mara mbili udiwani Kata ya Chang’ombe bila ya mafanikio na alipotaka
kugombea Kata ya Majengo akashindwa kwenye kura za maoni ndani ya chama.
“Kama alipitishwa kuwa mgombea angethubutu kuonesha ushahidi
wake wa maandishi,” amesema Muhoja na kusikitika kuwa siasa za kilaghai hazina
maana yoyote.
Kigaila naye amemkana Zoya kwamba si kampeni meneja wake na
hakuna kikao cha ngazi yoyote Chadema kilichompitisha.
Kuhusu tuhuma za kutishiwa kwa Zoya, Kigaila alisema hakuna mtu
anayeweza kumtishia Zoya kwa sababu chama ni taasisi na si mtu.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni