NEC-HAKUNA GOLI LA MKONO,LA SEMA KILA MTU ATAVUNA ALICHOPANDA,SOMA HAPO KUJUA
TUME ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) imesema, Watanzania na wanasiasa nchini hawana sababu ya kuwa na
wasiwasi kwa kuwa, hakutakuwa na goli la mkono. Anaandika Yusuph Katimba … (endelea).
“Ni uchokozi tu, hakutakuwa na goli la mkono
zipo sheria, taratibu na kanuni na hizi ndio zitakazofuatwa. “Kwenye Tume ya
Uchaguzi hakuna goli la mkono, vyama vyote visiwe na wasiwasi.
“Huku hakuna njia
ya mkato. Nilisema, wanaosema kura zitaibiwa, watuambie ili tuzibe mianya
hiyo,” amesema Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva leo jijini Dar es
Salaam alipokutana na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.
Akizungumzia
maandalizi ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu Lubuva amesema
maandalizi yanaendelea. “Mpaka tarehe 15 mwezi huu vifaa vyote tunatarajia view
vimefika katika maeneo husika,” amesema.
Hata hivyo
amevikumbusha vyama vya siasa kukumbuka kuzingatia maadili ili kuepusha nchi na
ghasia zozote zinazoweza kutokea.
“Maadili
yatawale katika uchaguzi mkuu. Kila chama kikizingatia maadili, sheria na
kanuni za uchaguzi amani itaendelea,” amesema na kuongeza;
“Vyama vyote
view tayari kuzingatia sheria na mshiriki yoyote awe tayari kukubali matokeo ya
uchaguzi yatakayotangazwa na tume.”
Akizungumzia watu
ambao hawataona majina yao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa njia ya
kielekroniki (BVR), Kamishna wa NEC, Jaji John Mkwawa amesema busara
itatumika ili kupata haki hiyo.
“Tumepitia na
tumeshughulikia kwa kiasi kikubwa. Ukifika kwenye kituo na hati ya kupigia
kura, itatazamwa ili kuangalia uhalali wake na baada ya hapo hekima itatumika
ili mtu huyo asikose haki yake ya kupiga kura,” amesema.
Katika hilo Jaji
Lubuva aliongeza kuwa lengo zima la uhakiki ni kujua ni wapi kuna tatizo na
kwamba, watu wa namna hiyo wakiwepo watapata msaada na wataweza kupiga kura.
Hata hivyo Jaji Lubuva amevitaka vyombo vya habari kusimamia
maadili ya uandishi ili kutoa usawa na kuwatendea haki wananchi pamoja na
wagombe wa vyama mbalimbali vya siasa nchini.
“Kwenye uchaguzi
haitakiwi kuegemea popote. Mtakuwa hamjawatendea haki wananchi kama mtaegemea
upende mmoja,” anasema Jaji Lubuva na kuongeza;
“Ili kila watu
ashiriki Tume ya Uchaguzi inaomba kuhamasisha wananchi kwa ujumla. NEC inaomba
kutumia kalamu ili watu waone umuhimu wa kutunza kadi zao.”
Jaji Lubuva
alilalamika kwamba wakati wa kuandika wapiga kura kwenye BVR, waandishin
walikuwa wakiripoti habari alizoziita kuwa hasi ikiwa ni pamoja na upungufu
wake.
Hata hivyo,
Katibu wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Nevile Meena alimweleza Jaji Lubuva
kuwa, vyombo vya habari vilijitahidi kuonesha kasoro hizo ambazo baadaye
walizifanyia kazi na kuwa, angepongeza kazi hiyo.
Habari hii
kwa hisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni