Zinazobamba

NEC YAMTULIZA JOHN MNYIKA,NI KUHUSU DAFTARI LA KUPIGA KURA SOMA HAPO KUJUA


TUME ya  Taifa ya Uchaguzi nchini NEC imesema majina ya wapiga kura yaliyopo kwenye Daftari la kupiga kura yatabandikwa kwenye vituo vya kupiga kura siku nane kabla ya siku ya kupiga kura ya octoba 25 mwaka huu.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
         Kuibuka huku kwa NEC kunakuja siku moja kupita baada ya Naibu Katibu mkuu bara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, John Mnyika kuitaka tume hiyo kupeleka Daftari hilo kwa wananchi mara moja,lasivyo wangeandamana hadi ofisi za NEC.
       Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Uchaguzi kutoka ndani ya NEC,Profesa Chaliga amesema Tume yake imesikitika juu ya tuhuma anazotoa Mnyika kuhusu Daftari hilo huku akisema kanuni za uchaguzi,
   Ni kwamba majina ya wapiga kura yanabandikwa kwenye vituo vya kupiga kura siku nane kabla ya siku ya uchaguzi.
        Amesema nia ya kubandika majina hayo siku nane kabla ni kuweka usalama ili yasibanduliwe.
        “Jamani anavyosema tunabandike leo kwenye vituo ni makosa kwani tukiyandaika leo mpaka siku yenyewe  ya kupiga kura si yatakuwa yamebanduka,ndio maana tunaweka siku nane kabla,kwahiyo wanasiasa wasipotoshe hili”
      Profesa Chaliga amesema kwa sasa hatua zinazoendelea ni tume hiyo kupeleka daftari hilo kwenye mikoa tofauti nchini.

       Naye Mwenyekiti wa NEC Jaji mstaafu Damian Lubuva amewataka watanzania ,kujitokeza siku ya kupiga kura  na kuwachagua viongozi wanaowataka baada ya hapo wanatakiwa kurudi nyumbani na kuacha kukaa kwenye vituo vya uchaguzi kwa madai ya  kulinda kura,amedai  katika uchaguzi huu hakuna kura yeyote itakayoibiwa.

Hakuna maoni