Zinazobamba

BREAKING NEWS-MAHAKAMA KUU YAMPUNGUZIA ADHABU MRAMBA NA YONA,NI BAADA YA RUFAA YAO,SOMA H

IMG_3632
          

NA KAROLI VINSENT
HATIMAYE mahakama Kuu imewapunguzia adhabu mawaziri wa wa awamu ya tatu ambao ni Waziri wa fedha Basil Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wa serikali ya awamu ya Tatu Daniel Yona toka miaka mitatu  jera  waliohukumiwa mwanzo, hadi miaka miwili.
     Hukumu hiyo imefuata baada mahakama hiyo chini Hakimu Protas Rugazia kutupilia mbali rufaa iliyotaka washitakiwa hao kuachiwa huru na badala yake wamepunguziwa adhabu kutoka hukumu ya miaka 3 na fidia ya shilingi milioni 5 katika mahakama ya mkaazi Kisutu ambapo sasa wote kwa pamoja wanatakiwa kwenda jera miaka miwili kila mmoja.



      Aidha Hakimu Rugazia amesema hatua ya kuwapunguzia adhabu imefuata baada ya kujiridhisha kuwa adhabu iliyokuwa imetolewa mwanzoni haikulingalina na uzito wa kosa walilotenda.
Mpaka mtandao huu  unaondoka mahakamani hapo mawakili upande wa washitakiwa hao hawakuwa tayari kuizungumzia hukumu hiyo
Bazir Mramba na mwenzake Daniel Yona walikuwa wanatuhumiwa kwa kosa la matumizi mabaya ofisi ya umma ambapo waliisababibishia serikali hasara ya shilingi Bilioni 11.7.



Hakuna maoni