WENJE NA NYERERE WAICHACHAFYA CCM MWANZA,WAUNDA UTATU MTAKATIFU,SOMA HAPO KUJUA
MGOMBEA Ubunge
wa jimbo la Nyamagana, Ezekia Wenje (Chadema), amesema Serikali ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) imechangia kuiuwa elimu na imeshindwa kutafuta mbinu na
mikakati ya kuikomboa isiangamie. Anaandika Moses Meseti, Mwanza … (endelea).
Kauli
hiyo aliitoa juzi wakati wa mkutano wa hadhara, uliofanyika katika viwanja vya
Bendera Tatu, Kata ya Bugarika, Nyamagana jijini hapa na kuhudhuliwa na
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara, Vicent Nyerere.
Wenje ambaye
pia ni Waziri kivuli wa Mambo ya Ndani, amesema kuwa kitendo cha serikali ya
CCM kuendelea kushusha madaraja ya ufaulu kuanzia elimu ya msingi na sekondari
imesababisha Taifa kuendelea kushuka kielimu.
Amesema kuwa CCM
wanafanya kitendo hicho kwa manufaa yao binafsi na kuamini ndiyo itakuwa msaada
katika safari yao ya kisiasa ili kuwaaminisha watanzania elimu inayotolewa ni
bora kumbe ni chanzo cha kuongeza ujinga kwa watoto wa masikini.
Hata hivyo
amesema watanzania wanapaswa kuwapa kura za ndiyo wagombea wa Umoja wa Katiba
ya Wananchi (Ukawa) akiwamo, Edward Lowassa ili kuboresha mitaara ya elimu
nchini, na kuondoa ada za shule kuanzia `vidudu` hadi chuo kikuu.
Mgombea ubunge
Jimbo la Musoma Mjini, Vicent Nyerere (Chadema) amewataka watanzania kupuuza
propaganda za CCM za kuwadanya kuwa, mgombea Urais kupitia Chadema, Edward
Lowassa ni mgonjwa kwani sio sehemu ya wabeba vyuma na watunisha misuri.
“Kazi ya hao
wenzetu CCM ni uongo na aibu ya kushindwa uchaguzi huu ndo inayowasumbua na
sasa wamekosa hoja wameanza kuongea bila mpangilio na kuwaeleza watanzania
watawafanyia nini kazi yao ni kuwapuuza,” amesema Nyerere.
Nyerere ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara, amesema ni wakati wa mabadiliko kwa kuwa
watanzania walishachoka na ahadi za uongo zisizotekelezeka na kusababisha
watanzania kuendelea kuishi maisha ya duni.
Mmoja wa wananchi waliohudhulia mkutano huo, Edward Madale,
amesema kutokana na CCM kushindwa kuwatekelezea na kutatua kero zao umefika
wakati muafaka wa kuacha kukichagua.
Habari hii
kwahisani ya mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni