UFISADI WA KUTISHA SERIKALINI WAIBULIWA,PPRA YAONYESHA MABILIONI YA PESA YANAPOTEA KWENYE MIRADI HEWA SOMA HAPO KUJUA
NA NORA DAMIAN, DAR ES SALAAM
UKAGUZI maalumu uliofanywa na
Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa mwaka wa fedha
2014/15 umeibua ufisadi mkubwa katika wizara, idara, wakala za
serikali, halmashauri, taasisi na mashirika ya umma.
Katika ukaguzi
huo, Wizara ya Ujenzi imegundulika kuwa imefanya malipo hewa ya
Sh milioni 951.7 yaliyolipwa kwa
makandarasi kwa kazi ambayo haikufanywa, huku Wizara ya Maliasili ikiwa na malipo hewa ya zaidi ya Sh milioni 156 kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).
makandarasi kwa kazi ambayo haikufanywa, huku Wizara ya Maliasili ikiwa na malipo hewa ya zaidi ya Sh milioni 156 kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).
Wizara ya Ujenzi inayoongozwa na
mgombea urais wa CCM Dk. John Magufuli pia imesababisha hasara
ya Sh bilioni 124.8 ambazo ni malimbikizo ya riba iliyozalishwa
kutokana na kucheleweshwa malipo ya wakandarasi yenye thamani
ya Sh trilioni 5.3.
Katika ukaguzi
huo wa PPRA, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Kampuni ya
Reli Tanzania (TRL) ni miongoni
mwa taasisi 17 zilizofanya vibaya katika ununuzi na kuwa na viashiria vya rushwa katika baadhi ya miradi.
mwa taasisi 17 zilizofanya vibaya katika ununuzi na kuwa na viashiria vya rushwa katika baadhi ya miradi.
Kutokana na ufisadi huo, PPRA
imependekeza taasisi zilizohusika na malipo hayo zirejeshe fedha hizo
kutoka kwa wazabuni waliolipwa na kuwachukulia hatua za nidhamu
watumishi waliohusika na malipo hayo.
Akiwasilisha ripoti ya ukaguzi huo
jana, Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Matern Lumbanga,
alisema ukaguzi huo ulihusisha taasisi 80 zikijumuisha wizara,
idara zinazojitegemea, wakala za serikali, halmashauri
za Serikali za mitaa, taasisi na mashirika ya umma. Kwa mujibu
wa ripoti hiyo, mikataba 5,206 yenye thamani ya Sh bilioni 214.6
ilikaguliwa ambako kazi za kandarasi zilikuwa mikataba 345,
bidhaa mikataba 1,112, huduma za ushauri wa utaalamu 34, huduma
zisizo za ushauri wa utaalamu 1,041, ununuzi yenye thamani ndogo
2,671 pamoja na matumizi ya utaalamu wa ndani mikataba mitatu.
Balozi Lumbanga alisema taasisi 35
zilifanyiwa ukaguzi kupima kama thamani bora ya fedha ilipatikana
kwenye miradi 186 yenye thamani ya Sh bilioni 296.
“Ukaguzi huo ulibaini ucheleweshaji
mkubwa wa malipo kwa wakandarasi hususan kwenye miradi ya ujenzi
wa barabara na miradi ya maji katika Serikali za Mitaa.
Sababu kubwa ni
kutokana na ucheleweshaji wa utoaji fedha zilizotengwa kwa ajili
ya miradi husika.“Ikumbukwe
kwamba malimbikizo ya riba yataendelea kuongezeka hadi hapo malipo yatakapofanyika.
kwamba malimbikizo ya riba yataendelea kuongezeka hadi hapo malipo yatakapofanyika.
Unapochelewesha
malipo ya wakandarasi halafu yanazaa riba maana yake Taifa linabebeshwa
mizigo ambayo
haistahili,” alisema.
haistahili,” alisema.
“Kati ya miradi 186 iliyokaguliwa,
miradi 35 yenye thamani ya Sh bilioni 58.2 ilipata wastani
usioridhisha wa chini ya asilimia 50.
“Hii ni ishara kwamba malengo
yaliyokusudiwa kwenye miradi hiyo kwa kiasi kikubwa hayatafikiwa
na thamani bora ya fedha inaweza isipatikane.
“Miradi 55 yenye
thamani ya Sh bilioni 81.26 ilipata wastani wa kuridhisha wa zaidi
ya asilimia 75 wakati miradi 96
yenye thamani ya Sh trilion 2.8 ilipata wastani wa kati ya asilimia 50 na 75,” alisema Balozi Lumbanga.
yenye thamani ya Sh trilion 2.8 ilipata wastani wa kati ya asilimia 50 na 75,” alisema Balozi Lumbanga.
Alizitaja
taasisi 17 zilizofanya vibaya na alama zilizopata kwenye mabano kuwa
ni NEC (38), TRL (51), Tume ya Ajira
(53), Kituo cha Uwekezaji (51), Shirika la Madini la Taifa-Stamico (56), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (60), Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (56), Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda (42), Halmashauri
ya Wilaya ya Karatu (49), Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi (50) na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo (57).

Nyingine ni
Halmashauri za Kigoma (52), Misungwi (55), Iramba (52),
Nanyumbu (60), Kyela (60) na Mamlaka
ya Majisafi na Maji taka Lindi (60). “Taasisi hizi zilishakaguliwa miaka iliyopita na kupewa mapendekezo ya namna ya kuboresha ununuzi wao kwa mujibu wa sheria lakini zimeendelea kuyapuuza mapendekezo hayo na kuendelea kufanya vibaya,”alisema.

Malipo hewa
Balozi Lumbanga alisema taasisi
tisa zilibainika kufanya malipo hewa kwenye miradi yenye thamani
ya Sh bilioni 6.4.
“Ukaguzi umebaini malipo ya ziada
ya Sh milioni 951.7 yalilipwa kwa wakandarasi kwa kazi hewa,
kiasi hiki ni sawa na asilimia 15 ya thamani ya miradi yote ya kazi
za ujenzi iliyokaguliwa,” alisema. Mwenyekiti huyo alizitaja
taasisi zilizohusika na malipo hewa kwenye mabano kuwa ni Shirika la
Hifadhi za Taifa – Tanapa (Sh milioni 156.3), TRL (Sh
milioni 473.6), Halmashauri ya Kigoma (Sh milioni 11.1),
Halmashauri ya Kibondo (Sh milioni 64.9), Halmashauri ya Jiji
la Mwanza (Sh milioni 69.6), Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi
(Sh milioni 55.6),
Halmashauri ya
Wilaya ya Tarime (Sh milioni 25.42), Halmashauri ya Wilaya
ya Rungwe (Sh milioni 93.09)
na Halmashauri ya Wilaya ya Kyela (Sh milioni 2.08).
na Halmashauri ya Wilaya ya Kyela (Sh milioni 2.08).
Pia alisema
ulifanyika uhakiki wa malipo hewa yaliyobainishwa kwenye ukaguzi
wa mwaka 2013/14 na kubaini malipo hewa ya Sh milioni
377. Kuhusu ucheleweshaji wa malipo, alisema mikataba 301 ya
Wakala wa Barabara (Tanroads), yenye thamani ya Sh trilioni 5.3
ilicheleweshewa malipo na hivyo kuwa na malimbikizo ya riba ya Sh
bilioni 124.8 hadi kufikia Juni mwaka huu.
bilioni 124.8 hadi kufikia Juni mwaka huu.
Rushwa kwenye ununuzi
Kulingana na
PPRA, taasisi inapopata asilimia 20 au zaidi katika
viashiria vya rushwa ni dalili ya kuwapo vitendo vya rushwa
kwenye ununuzi au miradi husika. Kulingana na ripoti hiyo,
katika miradi yote
186 iliyokaguliwa, miradi 27 ilibainika kuwa na viashiria vya rushwa kwa zaidi ya asilimia 20 na tayari Taasisi ya Kuzuia ya Kupambana na Rushwa (Takukuru) imearifiwa ichukue hatua zaidi.
186 iliyokaguliwa, miradi 27 ilibainika kuwa na viashiria vya rushwa kwa zaidi ya asilimia 20 na tayari Taasisi ya Kuzuia ya Kupambana na Rushwa (Takukuru) imearifiwa ichukue hatua zaidi.
Taasisi tisa
zilizobainika kuwa na viashiria vya rushwa ni NEC (asilimia 29),
TRL (22), Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (21), Halmashauri
ya Wilaya ya Mpanda (22), Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo
(24), Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma (28), Halmashauri ya
Wilaya ya Mbozi (20), Halmashauri ya Wilaya ya Karatu (31) na Agricultural
Input Trust Fund (28).
Input Trust Fund (28).
Alipotakiwa
kutoa ufafanuzi ni miradi ipi iliyokuwa na viashiria vya rushwa
katika NEC, Ofisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dk. Laurent Shirima
alisema: “Huwezi kutoa taarifa za uchunguzi wowote unaoendelea
hadi uwe umekamilika.
“Hatuwezi kutoa taarifa zozote kwa sababu kwa mazingira ya sasa hivi kuna vitu ambavyo huwezi kuvifanya…vinaweza kuwa na madhara au athari kwa jamii”.
“Hatuwezi kutoa taarifa zozote kwa sababu kwa mazingira ya sasa hivi kuna vitu ambavyo huwezi kuvifanya…vinaweza kuwa na madhara au athari kwa jamii”.
Hatua zilizochukuliwa
Balozi Lumbanga alisema maofisa
masuuli na wakuu wa vitengo wa taasisi 17 zilizofanya vibaya
na zilizotekeleza miradi 35 chini ya wastani wa kuridhisha,
watawajibika kujieleza mbele ya bodi hiyo kwa nini wasichukuliwe
hatua za nidhamu na sheria.
“Mamlaka itachukua hatua ya
kuwafungia wakandarasi na wataalamu washauri waliohusika na
malipo hewa. Taasisi zote zilizobainika kuwa na viashiria vya
rushwa zitawasilishwa Takukuru kwa uchunguzi zaidi.
“Tutapeleka timu
ya wataalamu kuhakiki malipo hewa ya wakandarasi kwa
kazi ambazo hazikufanywa,” alisema.
Pia alizitaka taasisi 53 zilizopata wastani chini ya asilimia 75 kuwasilisha PPRA mahitaji yao ya mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi na Kanuni zake.
Pia alizitaka taasisi 53 zilizopata wastani chini ya asilimia 75 kuwasilisha PPRA mahitaji yao ya mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi na Kanuni zake.
PPRA pia imezifungia kampuni saba
na wakurugenzi wake kushiriki zabuni za umma kutokana na
kukiuka mikataba waliyoingia na vitendo vya udanganyifu. Kati ya
kampuni hizo, sita zimefungiwa kwa miaka miwili na
moja imefungiwa kwa miaka 10 kwa kuwasilisha dhamana za zabuni
za kughushi wakati wa michakato ya zabuni.
Chanzo ni Gazeti la Mtanzania
Hakuna maoni
Chapisha Maoni