NEC KUVURUGA UCHAGUZI,BABU DUNI AIBUA MAZITO,SOMA HAPO KUJUA
Mgombea Mwenza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa mwanvuli wa Ukawa, Juma Duni Haj |
UMOJA wa Katiba
ya Wananchi (Ukawa) unaoundwa na vyama vinne vya upinzani vimedai kubaini
mchezo mchafu ambao unataka kufanywa na serikali ya CCM kwa kushirikiana na
Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC). Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Hali
hiyo imejitokeza kutokana na kile kinachodaiwa kuwa NEC imetoa takwimu za
upotoshaji ambazo zinalenga kuwapa ushindi CCM na kutimiza adhima yao ya ushindi
wa goli la mkono.
Kauli hiyo
ilitolewa jana na Mgombea Mwenza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
kwa mwanvuli wa Ukawa, Juma Duni Haji alipokuwa akizungumza na waandishi mjini
hapa.
Mgombea huyo
alisema kuwa takwimu zilizotolewa na NEC hazina ukweli wowote na kuna kila
sababu ya kutolewa ufafanuzi takwimu hizo wamezipataje.
Amesema kwa mujibu wa
tume ya uchaguzi inaonesha watu ambao wanastahili kupiga kura ni milioni 23.7
na vituo vyote vya kupigia kura vitakuwa ni 72,000 na kila kituo kitakuwa na
watu 450.
Amesema katika
kufanya ujanja ujanja NEC inaonekana kuwa na wapiga kura hewa milioni tisa
ambapo kuna vituo hewa 20,000 kwa ni vituo halisi vinatakiwa kuwa 53,000 na
siyo 72,000.
Mbali na hilo
Haji alifafanua kuwa kwa hesabu ya kuwa na vituo 72,000 kama hesabu ya Tume
inavyoelekeza ni wazi wapiga kura wanatakiwa kuwa milioni 32 na siyo milioni 23
tena.
Kutokana na hali
hiyo Duni amemtaka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Damian Lubuva
kuhakikisha anatoa mchanganuo mzuri wa mahesabu ya wapiga kura vituo utoa.
“Kamwe hatuwezi
kukubali tume kwa kushirikiana na serikali kutafuta ushindi wa goli la mkoni
kama ilivyozoeleka kwa chama hicho.
“Hata hivyo
natahadharisha serikali ikilazimisha kutaka inachokitaka wao, bila kusikiliza
watu wanataka nini, ni wazi kuwa kunaweza kutokea machafuko kwani watanzania
kwa sasa wamechoka na wanataka mabadiliko,” alisisitiza Duni.
Akizungumzia
kuhusu safari zake, amesema mpaka sasa kafanya mikutano katika majimbo 130
ambayo mengi yao yapo vijiji na watanzania wanamalalamiko yanayofanana.
Amesema wananchi
wamechoshwa na manyanyaso kwani wamekuwa wakimbizi katika nchi yao na mbaya
zaidi wananyanyaswa na wazawa wenzao na wala siyo wageni.
Amesema
watanzania wamechoshwa na mipango isiyokwisha ambayo uchangishwa kwa lazima
bila kuona mabadiliko yoyote ya ambayo wanatakiwa kuyapata.
Alimesema
watanzania wengi wanakumbwa na huduma mbovu ya afya, elimu, miundombinu,
ukosefu wa walimu mashuleni pamoja na shule nyingi kukosa madawati.
Mbali na hilo alieleza kuwa amebaini kwamba wanachi wengi hawana
uhuru kwa kufanya kile wanachokitaka kutokana na watawala wengi kuwatisha
wananchi.
“Inasikitisha
jinsi askari wanyama pori wanavyowashambulia wananchi hususani wale wanaoishi
karibu na hifadhi jambo ambalo linaanyima haki wananchi kufanya maamuzi,”
amesema Duni.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni