Zinazobamba

UTATA WAIBUKA GAZETI LA MTANZANIA KUTOONEKANA MTAAN LEOI,MHARIRI WAKE ANG'AKA,SOMA HAPO KUJUA

Gazeti la Kiswahili linaloongoza Tanzania

UTATA mzito umeibuka kuhusu kutoibuka leo mtaani Gazeti linalotoka kila siku la Mtanzania.(Mtandao huu umedokezwa).Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
          Maswali mengi yaibuka mtaani husasani kwa wauza magazeti pamoja na wasomaji ambao wengi walikuwa wananufaika na Gazeti hilo pendwa kwa sasa hapa nchini na wamekuwa na maswali mengi kutonekana leo.
      Kwa mujibu wa mtoa taarifa wa Fullhabari.blog aliyoko ndani ya ofisi la Gazeti la Mtanzania ameuambia mtandao huu kuwa gazeti hilo halijatoka mtaani kwasababu ilichapisha habari moja kubwa ambayo ilyoonyesha ubadilifu mkubwa wa fedha za umma ndani ya Serikali ambayo yalibuliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa mwaka wa fedha 2014/15

Chanzo chetu hicho kimezidi sema kuwa Gazeti hilo lilitoka ila  inadaiwa nakala zake zote zilinnuliwa zote ili zisifike kwa wananchi bila hata kumtaja aliyenunua nakala hizo,ambapo ndio maana Gazeti hilo alijatoka kabisa siku ya leo ya tarehe 7-10-2015,
 Huku Gazeti hilo likionekana mtandaoni likiweka habari hiyo kama unavyoona mchoro ambapo ilitakiwa iwe kwenye ukrasa wa mbele  
   mtz1
  WAUZA MAGAZETI WAFUNGUKA
Katika kuthibitisha madai hayo mtandao huu ulijalibu kuongea na wauza magazeti katika mkoa wa Dar es Salaam kutaka kujua je kwa siku ya leo wamepata nakala za Gazeti hilo,
Joseph Elias ambaye anauza magazeti maeneo ya Posta jijini hapa amesema hata wao wanashangaa kwanini leo gazeti la Mtanzania alijafika kwa mawakala ambao wanawapa magazeti ili wayauze.
      “Ujue mimi mwenyewe nimeshangaa huwaga haijawi kutokea Gazeti hili kutofika mtaani labda liwe limefungiwa lakini hili alijafungiwa kwahiyo tumeshangaa sana,yaani biashara zetu leo ziko vibaya,kwani gazeti hili linatuingizia pesa sana’amesema
      MHARIRI WA MTANZANIA ANENA
Fullhabari.blog ilijalibu kumtafuta mhariri wa Gazeti hilo Aradia Peter, kutaka kujua juu ya taarifa hizo, ambapo naye alishangaa mwandishi wa habari hizi amezipata wapi taarifa hizo ambapo ndipo akasema Gazeti la Mtanzania alijatoka leo barabarani kwasababu ya mtambo wa kuchapishia Gazeti hilo kuharibika dakika za mwisho,
“Hizo taarifa ni za uongo kwani Gazeti la Mtanzania alijatoka leo kwasababu ya mashine zetu za kuchapishia kupata itilafu kidogo ndio maana alijatoka”
Mwandishi wa Fullhabari.blog amkambana juu ya majibu yake  hayo kwamba,kama mashine zilikuwa na itilafu mbona Gazeti la michezo la Dimba ambalo nalo linatumia mitambo hiyo limechapishwa na liko mtaani?akajibu kwa kusema
“Mbona kama ndio hivyo Gazeti limetoka maeneo ya Kanda ya ziwa ambapo kuna mashine zengine”













Hakuna maoni