TAASISI YA CARE$ HELP YAJA NA HICHI KWA VIJANA ,SOMA HAPO KUJUA
TAASISI ya Care
& Help kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) na Tume ya
Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya Tanzania, imewataka Watanzania kuongeza
nguvu ya ziada katika kusimamia maisha ya vijana wa kike na kuboresha maisha
yao.
Hayo yamesemwa leo katika mjadala wa kongamano
la kujadili changamoto zinazowakabili wanawake lililofanyika chini ya taasisi
isiyo ya kiserikali ya Care and Help inayolenga kumkomboa msichana katika
majanga hayo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Uradibishi katika
TACAIDS, Jacob Kayombo amesema matatizo mengi ya wasichana yanatokana na mfumo
wa utamaduni usiompa haki ambazo hupelekea vishawishi.
Kayombo amesema miongoni mwa utamaduni mbovu uliojengeka ni
mwanamke kushiriki shughuli zinazoingiza kipato kidogo na kupigwa na hata
kusababisha ulemavu.
Amesema kuwa wanawake wakipewa elimu ya haki na usawa
itabadilisha maisha yao hivyo kuwa katika nafasi nzuri na kuepuka vishawishi
malimbali.
Pichani ni Ofisa Elimu wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za kulevya,Moza Makumbuli akizungumza kwenye Seminia hiyo
Makumbuli amesema kuwa licha ya uwezekano mkubwa wa wanawake
kuathirika lakini kwa sasa tiba yao inapatikana katika hospitali za mikoa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni