LOWASSA NA MAGUFULI WAMTISHA MKURUGENZI WA TANESCO ATANGAZA KUMALIZA MGAO WA UMEME NCHI NZIMA,SOMA HAPO KUJUA
Mkurugenzi wa shirika la ugavi wa umeme nchini TANESCO Felchesmi Mramba |
NA KAROLI VINSENT
SIKU moja kupita baada ya wagombea wa
Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ambaye anaungwa mkono
na vyama vya UKAWA Edward lowassa pamoja na Mgombea Urais kupia CCM John
Magufuli,
kumtishia kumfukuza kazi mkurugenzi wa shirika
Shirika la umeme nchini TANESCO endapo moja wao akiingia madarakani, kwasababu
ya mgao wa umeme unaoendeleo nchini
Hatimaye sasa Mkurugenzi huyo wa TANESCO ameibuka na kuwahakikishia watazania
kuwatatizo la kukatika kwa umeme litakuwa limekwisha ndani ya wiki hii, na kurejesha umeme katika hali yake ya
kawaida.
Akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam mkurugenzi wa tanesco Felchesmi Mramba amesema
mpaka jana wamefanikiwa kuwasha mtambo wenye megawati 35
unaomilikiwa na kampuni ya Symbion,ambao kwa kiasi kikubwa umeongeza
nguvu katika gridi ya taifa na baadhi ya maeneo yamekuwa yakipata umeme
wa uhakika.
Aidha amesema Tanesco inafahamu
hali ngumu ya kukatika kwa umeme wanayo kumbana nayo wananchi katika
mikoa ya arusha,Mwanza,Kilimanjaro,Mbeya,Dodoma,na kwingineko ambapo amewaomba
radhi wananchi na kuwataka waendelee kuwa na subira wakati shirika hilo
likiendelea kurekebisha hali hiyo.
Pia amefafanua kuwa hali katika
mabwawa ya kuzalishia umeme wa maji sio nzuri mara baada ya kupungua kwa
asilimia 81.3 na hivyo husababisha ukosefu wa umeme.
Mkurugenzi huyo ameeleza
kupatikana kwa umeme wa gesi kutaendelea kukuza na kuboresha hali ya
umeme nchini na kusisitiza Tanesco itaendelea kutoa taarifa kila
wiki ili kuwapa wananchi taarifa jinsi hali inavyoendelea .
Hata hivyo amesema shirika hilo ndani ya
wiki hii linatarajia kupata kiasi kingine cha umeme ambapo megawati
70 kutoka Kinyerezi megawati 20 kutoka Syimbion.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni