OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU KUPIMA VIASHIRIA VYA MAELENGO ENDELEVU(SDGs)SOMA HAPO KUJUA
Ofisa Habari wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa ,Veronica Kazimoto |
OFISI ya Takwimu
Taifa inatarajiwa kufanya mkutano utakaokusanya wadau wa takwimu kujadili jinsi
ya kupima viashiria vya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs), utakaofanyika
oktoba 8, 2015.Anaandika KAROLI VINSENT
endelea nayo
Hayo yamesemwa na Ofisa Habari wa Ofisi ya
Takwimu ya Taifa ,Veronica Kazimoto alipozungunza na waandishi wa habari leo
Jiji Dar es Salaam.
Amesema kuwa, takwimu hizo zitawezesha taifa kupima utekelezaji
wa malengo ya maendeleo endelevu na mipango mengine kama mpango wa maendeleo wa
Tanzania 2025 na kwamba, mkutano huo utakuwa na mijadala mahususi ya kujadili
na kuhakiki takwimu za viashiria vya mpango huo.
Mkutano huo utahudhuriwa na wadau zaidi ya 100 kutoka katika
Wizara, Idara, Wakala na Taasisi ambapo mgeni rasmi atakuwa Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Amesema kuwa, kabla ya nchi wakuu wa nchi kujadili kukuwa kwa
maendeleo, kulikuwa na mpango wa malengo ya millenia ambayo nchi nyingi za
Afrika ikiwemo na Tanzania hazikufika malengo yote kwa ukamilifu hivyo Ofisi ya
Takwimu itakuwa sehemu ya kuchochea kasi ya kutimiza malengo hayo.
Aidha malengo hayo yalifikiwa nchini Marekani baada ya wakuu wa
nchi mbalimbali kujadili Mpango Mpya wa Maendeleo Endelevu wenye malengo 17
(SDGs) kufuatiwa kumalizika kwa Malengo ya Mellenia (MDGs) ambao utekelezaji
wake ulikuwa kwa miaka 15 (2000- 2015). Mpango huu mpya utaanza mwaka huu hadi
2030.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni