Zinazobamba

HABARI ILIYOWAHUZUNISHA WANANCHI WA ZANZIBAR LEO HII HAPA,SOMA HAPO KUJUA

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha (kushoto) akifafanua jambo
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha (kushoto) akifafanua jambo

MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametangaza kufuta matokeo ya uchaguzi wa kisiwani humo bila kutoa sababu za kufanya hivyo. Anaandika Jabir Idrissa, Zanzibar … (endelea).
     Jecha ametangaza tangazo hilo kupitia Shirika la Habari la Zanzibar (ZBC) na kuacha sintofahamu kwa wananchi wa Zanzibar wasijue nini cha kufanya.
          Jecha hakuwepo katika ukumbi wa kufanya majumuisho ya kura za Urais wa Zanzibar bila kutoa taarifa yoyote.
Majukumu ya kufanya majumuisho ya kura yalikuwa yakisimamiwa na Makamo Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Adbulhakim Issa Ameir ambaye naye alitekwa muda mchache kabla ya tangazo hilo kutolewa.
        Jaji Ameir alikuwa akisimamia majumuisho hayo, lakini aliitwa nje na kuchukuliwa na askari wa FFU na kupelekwa pasipojulikana na muda mchache ujao ikatangazwa taarifa hiyo.


Maoni 3

Bila jina alisema ...

HAKUUMIA MAALIM SEIF PEKE YAKE BALI TUMEUMIA WATANZANIA WOTE WAPENDA HAKI VISIWANI NA HUKU KWETU TANZANIA BARA.MAALIM SEIF ALIKWISHA SHINDA UCHAGUZI HUU.AMEFITINIWA.KUFUTWA MATOKEO WAKATI NI SIKU YA MWISHO YA MAJUMUISHO?TATIZO NI CCM.HAWAJAJIANDAA KISAIKOLOIA,YAANI WAKUBALI KWAMBA WATANZANIA WAMEKWISHA WACHOKA.URUDIWE UCHAGUZI?HAPANA.MWENYE KUSTAHIKI-MPENI CHAKE.UMAARUFU WA MAALIM ZANZIBAR UNAZIDI KUPANDA.HITIMISHENI,MPENI MAALIM HAKI YAKE YA KUITAWALA ZANZIBAR,NI MSHINDI HALALI,AMESHINDA UCHAGUZI.

Bila jina alisema ...

TANGU MATOKEO YA KURA ZA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR YALIPOANZA KUTANGAZWA JUZI TAREHE 26 GAZETI LA CCM UHURU LIMEKUA,KWA MBWEMBWE NYINGI LIKIMSIFA MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKETI YA CCM DR.ALLY MOHAMED SHEIN KWAMBA ANAONGOZA NA AMEMUACHA MBALI MGOMBEA WA CUF-UKAWA MAALIM SEIF SHARRIF HAMAD.WAATI HUO WOTE WALIKUA WAKITOA MATOKEO KWA MAJIMBO YA UNGUJA TUU.GHAFLA LEO TAREHE 28,UPEPO UMEBADIRIKA.INABIDI MATOKEO YA PEMBA [HATIMAYE-]YASOMWE.MUNGU WANGU WEE,EEE MUNGU BABA,YARABI TOBA,MUNGU WA IBRAHIM NA ISAYA NA YAKOBO MAALIM SEIF AMECHOMOZA MSHINDI,TENA WA WAZI BILA SHAKA SERIKALI SASA SIJUI YA MUUNGANO AU YA MAPINDUZI ZANZIBAR INAMUAMURU MWENYEKITI WA NEC AFUTILIE MBALI HESABU ZOTE,NA KUMBUKUMBU KWAMBA UMEFANYIKA UCHAGUZI.LINAWEZEKANA HILI KWELI?KUFUTA UCHAGUZI?ILI IWEJE? NANI AONGOZE ZANZIBAR MAANA MUDA IKATIBA NDIO UNAKWISHA WIKI HII.DUNIA ITUSAIDIE.SERIKALI YA TANZANIA IMETIA DOA LA KARNE KATIKA KUHESHIMU UTAWALA WA KIDEMOKRASIA.NI AIBU KUBWA MNO,AIBU,SHAME-UPON.

Bila jina alisema ...

NI MWENYEKITI WA ZEC [ZANZIBAR] JECHA SALIM JECHA NDIYE ALIYEPEWA TAARIFA AISAINI NA AISOME,APENDE -ASIPENDE.HUYU MWENYEKITI WA NEC JAJI DAMIAN LUBUVA AMESEMA YA ZANZIBAR HAYAWAHUSU,KASAHAU AMEKWISHA ISOMA ORODHA TA WABUNGE TOKA UNGUJA NA PEMBA! KIVUMBI!