WAANGALIZI WA TACCEO WATAJA KASORO KIBAO KWENYE UCHAGUZI,SOMA HAPO KUJUA
Mwenyekiti wa mtandao wa asasi zaidi ya 17 zinazoangalia chaguzi TACCEO Bi MARTINA KABISAMA akizungumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam |
Mtandao wa asasi za Kiraia wa kuangalia
chaguzi nchini Tanzania TACCEO ambao unaratibiwa na kituo cha sheria na haki za
binadamu LHRC ambao ni waangalizi wa ndani wa uchaguzi unaoendelea
nchini wamewataka wasimamizi wa uchaguzi ambao bado hawajatangaza matokeo ya
wabunge katika majimbo mbalimbali kufanya hivyo mara moja kwa kuwa
ucheleweshaji wa matokeo hayo unaweza kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani
katika maeneo hayo.
Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam kupitia
kwa mwenyekiti wa mtandao huo wa TACCEO Bi MARTINA KABISAMA wakati wakitoa
tathmini ya uchaguzi huo hadi sasa ambapo amesema kuwa ucheleweshwaji wa
kutangazwa kwa matokeo ya ubunge katika maeneo mbalimbali umekuwa ni changamoto
kubwa ambayo imekuwa ikisababisha kutumika kwa nguvu ya polisi pamoja na vurugu
kubwa kutokana na wananchi kukosa uvumilivu wa matokeo hayo.
Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi sura
namba 343 ya sheria za Tanzania katika kifungu cha 8(a) inatamka kuwa msimamizi
wa uchaguzi analazimika kutangaza matokeo ya uchaguzi mara moja pasipo
kuchelewa baada ya kukamilisha kujumlisha kura hizo,huku akisema taarifa
walizonazo kutoka kwa waaangalizi wao zinaonyesha kuwa kucheleweshwa kutangazwa
kwa matokeo ni katika majimbo zaidi ya 21.
Ametolea mfano baadhi ya majimbo ambayo tatizo hilo
lilijitokeza na kusababisha taharuki kubwa kuwa ni Temeke,Ilala,Simanjiro,na
Zanzibar ambapo kumekuwa na sababu mbalimbali zinazochangia ikiwemo wagombea
kudai kurudiwa kuhesabu kura,wagombea kukataa kusaini,kupotea kwa baadhi ya
nyaraka husika,kupotea kwa baadhi ya masanduku ya kura,kuchelewa kupokea vifaa
kutokana na changamoto za kijografia,ambapo hali ya kuchelewa huko
kumesababisha wananchi kukosa uvumilivu na kuhisi kuwa kuna mbinu chafu
zinazofanywa na kuamua kufanya fujo ikiwemo kuchoma baadhi ya ofisi za
serikali.
.
Kaimu Mkuruhenzi wa kituo cha sheria na haki za Binadamu LHRC Bi IMELDA LULU URIO akizungumza wakati wa kutoa report ya maendeleo ya uchaguzi wa mwaka huu nchini kwa mujibu wa waangalizi wao mbalimbali nchi nzima |
Aidha katika hatua nyingine mtandao huo umebaini
kuwepo kwa matumizi makubwa ya nguvu za dola kutoka kwa polisi kwa wananchi
wasio na hatia wanaofurahia matokeo yao ya ushindi,huku wakisema matumizi hayo
ya nguvu yanawafanya hata raia wema kuzoea vurugu na fujo na kuona kama
mchakato wa democrasia ni mchakato wa fujo na vurugu,ambapo amelitaka jeshi la
polisi kuhakikisha linatenda haki kipindi hiki
Hakuna maoni
Chapisha Maoni