CCM YAZIDI TITIA,MWENGINE ATOROKA,WENYE AKILI ZAO WAZID MSUSIA KIKWETE CCM YAKE,SOMA HAPO KUJUA
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Juma Mwapachu (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe |
ALIYEWAHI kuwa
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kada wa Chama cha Mapinduzi
(CCM), Balozi Juma Mwapachu leo ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho
kutokana na chama kupoteza dira.
Tamko
la Balozi Mwapachu ambalo amelithibitisha kutoka kwake, linasema kuwa kuanzia
kesho kada huyo wa CCM hatakuwa tena mwanachama wa chama hicho tawala na
kuongeza kuwa bado hajaamua kujiunga na chama kingine.
“Kuanzia kesho
mimi si mwana CCM tena. Nitarejesha rasmi kadi yangu kupitia ofisi ya CCM ya
kata yangu Mikocheni, Dar es Salaam. Kwa sasa sijaamua kujiunga na chama
kingine. Mwenyezi Mungu anilinde,” inasema sehemu ya tamko hilo.
Mwanasiasa huyo
ambaye amekuwa ndani ya CCM kwa miaka 48 sasa amesema kuwa katika mchakato wa
kumpata mgombea urais wa chama hicho, chama kilidhihirisha kutokuwa chama
kinachoendeshwa kwa misingi ya demokrasia kwa kumuengua waziri mkuu wa zamani,
Edward Lowassa ambaye anapendwa na wengi ndani ya chama.
Mwapachu amesema
kuwa Lowassa na wanachama wengine wa CCM waliojitoa ni sahihi hivyo naye
anaungana nao.
“Kujitoa kwake
uanachama wa CCM hivi karibuni ni sahihi kabisa kwa sababu CCM si chama tena
cha watu. Kimetekwa, na mimi nakubaliana na msimamo wa Lowassa na hao
waliyofuata kutoka ndani ya CCM,’’ amesema Mwapachu.
Mwapachu ameshika nyadhifa mbalimbali ndani ya chama hicho
lakini pia amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Habari hii
kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni