CCM WAIBIANA WENYEWE KWA WENYEWE PESA ZA KAMPENI,SONGOMBINGO LAANZA DODOMA,SOMA HAPO KUJUA
Mgombea Ubunge Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Dodoma Mjini. Kulia Mgombea Mwenza wa CCM, Samia Suluhu |
MGOMBEA Ubunge
jimbo la Dodoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Anthony Mavunde
anadaiwa kumdhurumu aliyekuwa kampeni meneja wake, Sospeter Mzungu fedha Sh.
3.6 milioni. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Mzungu amesema wakati wa kipindi cha mchakato
wa kura za maoni ndani ya CCM, walikubaliana na Mavunde aache kazi katika kituo
cha radio cha Ras FM kuwa kampeni meneja wake kwa malipo ya kiasi hicho cha
fedha.
Akizungumza katika uzinduzi wa mkutano wa kampeni za Chadema
uliofanyika kata ya kiwanja cha ndege Mzungu amesema Mavunde hafai kuwa mbunge
wa Dodoma Mjini kwani ni mtu ambaye haaminiki.
“Nilimwamini sana Mavunde, nilidhani anaweza kuwa kiongozi mzuri
lakini nimegundua kuwa ni mbabaishaji.
“Sababu za kutomwamini ni hivi, wakati wa mchakato wa kura za
maoni ndani ya CCM aliniomba niache kazi ili nimsaidie kumfanyia kampeni na
kuratibu shughuli mbalimbali ndani ya mchakato huo kwa makubaliano ya kunilipa
milioni 3.6 lakini hadi sasa ameamua kuzizika.
“Jamani wananchi nataka kuwaeleza wananchi kwamba iwapo
mtamchagua Mavunde ni wazi Dodoma itaendela kuwa nyuma kimaendeleo kwani ni mtu
ambaye ana ahadi nyingi ambazo hazitekelezeki,” amesema Mzungu.
Mbali na hilo amesema Mavunde amekuwa akitumiwa zaidi na Mamlaka
ya Ustawishaji makao Makao Makuu (CDA) ili kupanga mipango ya kuwabomolea
wananchi nyumba zao bila fidia.
Amesema kamwe Mavunde hawezi kukomesha manyanyaso ya ardhi kwa
mji wa Dodoma kwani ni sehemu yake ya ulaji.
Mwanahalisi Online ilimtafuta Mavunde kujibu tuhuma hizo, naye
amesema, ni kweli anafahamiana sana na Mzungu na ni rafiki yake, lakini
aliyosema hayana ukweli wowote.
“Ni kweli huyo jamaa (Mzungu) nafahamiana naye sana na ni rafiki
yangu sana, lakini nashangaa kusikia anatumia majukwaa kusema hivyo, kimsingi
nimekuwa naye lakini makubaliano hayakuwa hivyo kama anavyosema,” ameeleza
Mavunde.
Hata hivyo Mavunde hakuwa tayari kueleza makubaliano yake na
Mzungu yalikuwaje.
Kwa upande wake Mgombea Ubunge jimbo la Dodoma Mjini kwa tiketi
ya Chadema, Benson Kigaila amesema kipaumbele chake cha kwanza katika jimbo
hilo ni wananchi kumiliki ardhi.
Kigaila amesema wakazi wa Dodoma pamoja na mambo mengine
wanayokumbana nayo ni kukosa uhalali wa kumiliki ardhi yao.
Naye mgombea udiwani kata ya kiwanja cha ndege kupitia Chadema,
Pompi Mnyarapi amesema akichaguliwa atapambana na tatizo la mfumo wa elimu
pamoja na kukomesha michango mbalimbali ambayo wazazi wanachangishwa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni