GOLI LA MKONO- MYIKA ARUSHA KOMBORA JENGINE NEC,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John
Mnyika
NAIBU Katibu Mkuu wa
Chadema (Bara), John Mnyika ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kujibu hoja
zinazoibuliwa kuhusiana na Uchaguzi Mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Octoba 25
na sio kupotosha kwa makusudi huku ikiacha hoja za msingi zinazotolewa zikielea. Anaandika
Charles William … (endelea).
John Mnyika ambaye pia ni Mgombea Ubunge wa
Chadema katika jimbo la Kibamba, amezungumza hii leo jijini Dar makao makuu ya
UKAWA eneo la Ngome, na kusema Tume ya Uchaguzi mpaka sasa inastahili kutiliwa
shaka kwa kuwa inaweza kusababisha utata mkubwa kwa kuendelea kuchelewesha
daftari la wapiga kura kwa vyama vya siasa.
“Hatuwezi kuiacha Tume
iendelee kufanya ucheleweshaji wa kutoa orodha ya wapiga kura nchi nzima kwa
vyama ili wataalamu wetu wa teknolojia ya kompyuta wayahakiki, siku zimeshabaki
chache na tukumbuke mwaka jana muda kama huu vyama tulikuwa tumeshapewa ‘soft
copy’ ya daftari na kulifanyia uhakiki,” amesema Mnyika.
Mnyika ameitaka NEC
kutoa orodha ya wapiga kura wote mpaka kufikia siku ya Jumatatu wiki ijayo
(kesho kutwa) ili kuondoa sintofahamu inayoweza kujitokeza kutokana na daftari
hilo kucheleweshwa kwa Vyama kwa Vyama vinahitaji kuwapatia nakala ya daftari
hilo mawakala wao nchi nzima.
Katika hatua nyingine
Mnyika ameiasa NEC kuacha upotoshaji, kwa kusema busara ya wasimamizi wa
Uchaguzi inaweza kutumika kuwaruhusu watu wenye vitambulisho vya kupiga kura
watapiga kura hata kama wasipokuwepo katika orodha ya wapiga kura, huo ni
upotoshaji mkubwa.
“Tumesikia NEC
ikifanya upotoshaji ambao unakiuka sheria za uchaguzi kuwa wenye vitambulisho
ambao majina yao yatakosekana kwenye daftari busara inaweza kutumika wakapiga
kura. Huu ni upotoshaji na sheria inakataa kabisa, busara inaweza kutumika kwa
wale wenye utata wa vitambulisho lakini wapo kwenye daftari na si vinginevyo,”
amefafanua Mnyika.
Pia Mnyika amewataka
watanzania watakaohudhuria tamasha la kuiombea amani ya Tanzania siku ya kesho
wamuombee zaidi Rais Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva
kwani wao ndio watu muhimu wanaotakiwa kutenda haki na kufanya amani iendelee
kuwepo hata baada ya matokeo ya uchaguzi.
Mwanahalisi Online
ilijaribu kumtafuta Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhan Kailima
kwa njia ya simu ili kutolewa majibu baadhi ya hoja za Mnyika hata hivyo
hakupokea licha ya kupigiwa zaidi ya mara tatu na kutumiwa ujumbe mfupi wa simu
lakini hakuwa tayari kujibu pia.
Hapo awali Tume
iliahidi kubandika orodha ya wapiga kura katika vituo walivyojiandikishia siku
nane kabla ya uchaguzi ili kuwawezesha wananchi kuweza kuangalia majina yao na
kutoa malalamiko iwapo kuna dosari zozote zilizoonekana.
TAZAMA VIDEO YAKE HIYO HAPO
KUHUSU WANAHABARI
Hakuna maoni
Chapisha Maoni