KIKWETE AZIDI SUSIWA CCM YAKE,KINGUNGE ATOROKA CCM,AMCHANA CHANA KWA KUUA UCHUMI WA NCHI,SOMA HAPO KUJUA
Kada wa siku nyingi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru |
KADA wa siku nyingi
ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru ‘ametoroka’ chama
hicho kutokana na kile alichokieleza kimepoteza mwelekeo. Anaandika
Pendo Omary … (endelea).
Akizungumza
na waandishi wa habari nyumbani kwake leo jijini Dar es Salaam Kingunge
amesema, hatojiunga na chama chochote cha siasa “lakini kuanzia sasa mimi sio
mwanachama wa CCM,” amesema.
Katika mazungumzo yake na waandishi wa
habari, neno ‘mabadiliko’ lilitawala kinywa chake huku akionya kuwa, nguvu ya
kupinga mabadiliko ni kubwa.
“Nguvu ya kupinga mabadiliko ni kubwa
sana lakini kwa utafiti wangu mimi mzee ni kuwa, nguvu ya kuleta mabadiliko ni
kubwa zaidi. Watu wajiamini zaidi na wasubiri tarehe 25 Oktoba mwaka huu,”
amesema.
Akielezea namna CCM ilivyopoteza
mwelekeo Kingunge amesema chama hicho kimelewa madaraka kutokana na kutawala
kwa muda mrefu na kuongeza kuwa ‘wananchi sasa wanataka mabadiliko.”
Hata hivyo, kiongozi huyo aliyejiunga
na TANU siku saba baada ya kuanzishwa kwake na baadaye TANU na ASP ya Zanzibar
kuungana na kuanzisha CCM mwaka 1977 amesema chama hicho tayari kimeishiwa
pumzi.
“Kuongoza nchi ni kama kupanda mlima,
utafika mahala pumzi zinakwisha na huwezi kuendelea mbele na ukijaribu kwenda
mbele unabaki pale pale, na hivi ndivyo CCM ambapo kimeishiwa pumzi na kimebaki
pale pale hakiwezi tena kupanda mlima,” amesema Kingunge.
Baada ya kutangaza uamuzi wa kujiondoa
CCM, amesema hakusudii kujiunga na chama chochote, Ngingunge ameeleza kuwa
alipigana ndani ya CCM kutaka kuhakikisha chama hicho kinabaki salama kwa
kumchagua ama kumpitisha mtu aliye na sifa na kukubalika.
“Nilipigana nikiwa ndani ya CCM
kuangalia nani anafaa ili kuileta nchi kwenye mstari. Niliangalia ili kujua
ndani ya chama nani tukimpata anaweza kuipeleka nchi mbio.
“Nilimwona Edward Lowassa kuwa ana sifa
kuliko wengi waliojitokeza. Kiongozi lazima akubalike na watu, hii ni sifa
tangu wakati wa TANU,” amesema Kingunge na kuongeza;
“Lowassa anakubalika ndani ya CCM na
nje ya CCM, ni hivyo pamoja na kutangaziwa mambo ya ajabu kwa miaka minane
mfululizo.”
Lowassa ambaye alihama CCM na kujinga
na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alipitishwa na chama hicho
kuwania urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25
mwaka huu.
Chadema ni miongoni mwa vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ikiwa ni pamoja na Chama cha
Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.
Kabla ya kujiunga na chama hicho, ndani
ya Serikali ya awamu ya nne, Lowassa aliwahi kuwa Waziri Mkuu ambapo alijiuzilu
nafasi hiyo kutokana na kuhusishwa na kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya
Richmond.
Pia Kingunge ameshngazwa na hatua ya CCM
kutoa kauli zinazoonekana kung’ang’ania madaraka.
Amesema “kauli zinazotoka sasa hivi,
wapinzani hawawezi kushinda. Nyinyi mnajuaje kama hawawezi kushinda? Ukiritimba
wa chama kimoja kwa karne moja umetosha, madaraka hulevya.”
Akizungumiza chama tawala kuacha
utanaduni wake Kingunge amesema chama hicho kimeacha ‘itikio’ lake
lililoasisiwa tangu kuanzishwa kwa chama hicho.
“Wamebadilisha kauli mbiu ya chama
badala ya kidumu Chama Cha Mapinduzi – kidumu, sasa wanaitikia kidumu chama
tawala,” anasema na kuongeza; “niliwaambia NEC kwamba ukisema hivyo maana yake
wewe unataka kubaki kwenye utawala.”
Akimzungumzia mgombea urasi wa CCM,
Dk. John Magufuli, Kingunge amesema nafasi hiyo ameipata kutokana na chama
hicho kuvunja katiba ya chama.
Hata hivyo ameeleza kuwa, tatizo kubwa
la wananchi ni uchumi na ajira, “masikini uanondolewa na uchumi bora,” amesema.
Amesema, Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin
Mkapa aliacha uchumi ukikua kwa asilimia saba na kuingiza nchi kwenye orodha ya
nchini zinazokwenda mbio kiuchumi.
“Tazama, Kikwete (Rais Jakaya Kikwete)
kapokea uchumi ukikuwa kwa silimia saba na sasa ni miaka 10 uchumi unakuwa
karibu na asilimia saba -miaka 10 hii yote tumepiga make time na kiukweli
tumerudi nyuma. Mabadiliko ni muhimu ili upate watu wengine wenye pumzi mpya,”
amesema.
Habari hii kwahisania ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni