TNGP YAWAKABA KOO WANASIASA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU,SOMA HAPO KUJUA
Mkurugenzi wa TGNP Be Lilian Liundiakiwahutubia wanaharakiti mbali mbali wakati wa Tamasha la wanawake |
WITO umetolewa kwa Watanzania kuchagua viongozi ambao sera ya ilani ya vyama
vyao, itatatua kero zao na iwe yenye
kutekelezeka kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa na sio maisha binafsi.Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo
Wito
huo umetolewa wakati wa kilele cha Tamasha la Jinsia jijini Dar es
Salaam,tamasha hilo liloandaliwa kwa kushirikiana na Mtandao wa Kijinsia nchini
TNGP ambapo wanachi kutoka warsha mbalimbali walikuwepo ,wakito wito kwa pamoja
wamesema kuwa watanzania wanatakiwa kuwa
makini kwa kuwachagua viongozi ambao watawahaidi sera zinazo tekelezeka na sio
vinginevyo.
Wakitaja
baadhi ya matatizo ambayo yanawakabili ni pamaoja na suala la upatikanaji wa
hudma ya maji safi na salama maeneo mbali mbali nchini, hivyo watahakikisha
wanawauliza wagombea wa ngazi mbali mbali za uongozi ikiwemo udiwani, ubunge na
urais, ni kwa kiasi gani watashughulikia suala la huduma ya maji.
Vilevile wamesema chama kitakacho pata ridhaa ya
kuiongoza Tanzania kwa awamu ya tano, ifanye mabadiliko ya katiba ambayo
yataondoa mfumo kandamizi dhidi ya mwanamke , pia wameitaka tume ya taifa ya
uchaguzi (NEC) kutofumbia macho suala la matusi na kejeli zinazofanywa na
viongozi wa siasa katika kampeni zao, jambo ambalo linaweza chochea uvunjifu wa
amani nchini, huku wakiwataka tume kutenda haki kwa vyama vyote vinavyo shiriki
katika uchaguzi mkuu.
Wanaharakati wakimsikiliza kwa makini Be Liundi |
Hivyo wameitka serikali kutambua michango ya
kimaendeleo inayofanywa na iliyofanywa na wanawake kwa kuwawekea kumbukumbu
kama ilivyo kwa wanaume, ili kuleta uwiano wa kijinsia, pia wamesema
watahakikisha wanaishauri serikali kuandaa sera maalumu itakayo tambua mchango
wa wanawake na kuweka kumbukumbu katika
makumbusho maalum ya wanawake
Huku wakiwataka waandishi wa habari kutumia taaluma
yao kwa kutoa elimu ya uraia na masuala mbalimblai mtambuka yenye tija kwa maendeleo ya ukombozi wa taifa.
Tamasha hilo la kijinsia lililo andaliwa na wadau
mbali mbali wa masuala ya kijinsia kwa kushirikiana na mtandao wa kijinsia TGNP, limefikia kilele
leo jijini Dar es Salaam likibeba kauli mbiu ya mifumo kandamizi ya Mageuzi ya
mifumo kandamizi hayaepukiki.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni