TANZANIA YAANGUKIA PUA UWAZI WA BAJETI,YASHIKA NAFASI YA TATU AFRIKA MASHARIKI
LICHA ya serikali kutangaza kuweka wazi taarifa ambazo zinahitajiwa sana na wananchi ili kufanya ufuatiliaji na uwajibikaji wa serikali, Ripoti ya kimataifa imeonyesha kuwa Tanzania imeendelea kufanya vibaya kutokana na kutoa baadhi tu ya taarifa lakini taarifa za kibajeti bado ni changamoto.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo ofisini kwake, meneja utafiti na uchambuzi wa sera kutoka Haki elimu alisema hayo yalibainika baada ya ripoti kuu ya taifa kutolewa huku ikionyesha kwa ukanda wa Afrika mashariki ikishika nafasi ya Tatu.
Alisema katika ukanda huo, nchi ambayo imefanya vizuri kwa kutoa taarifa zake za kibajeti ni Kenya ikifuatiwa na Uganda na Tanzania kushika nafasi hiyo ya Tatu.
Kwa mujibu wa mtaalamu huyo alisema katika ripoti hiyo ya Kimataifa imeonyesha kuwa Tanzania ilipata alama 46 kati ya 100 katika kipimo cha uwazi wa bajeti kwa mwaka 2015, ikimaanisha kwamba serikali hutoa baadhi tu ya taarifa za bajeti kwa umma. kwa mujibu wa Ripoti hiyo Tanzania huweka wazi nyaraka 6 kati ya 8 muhimu zinazopaswa kuwekwa wazi kwa umma. hata hivyo taarifa ambazo zinawekwa wazi haziwasaidii wananchi kupata ujumbe kamili.
utafiti huo umefanywa katika nchi 102 duniani, utafiti huo wa mwaka 2015 umebainisha kuwa Tanzania inatakiwa kufanya maboresho zaidi ili iweze kutoka kundi la nchi lambazo ziko ngazi ya kati katika kipimo cha uwazi wa bajeti.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni