MAMLAKA YA ELIMU YAGUSWA NA CHUO KIKUU CHA SAYANSI CHA MWALIMU NYERERE,CHAIPIGA JEKI,SOMA HAPO KUJUA
MAMLAKA ya
Elimu nchini (TEA) imetoa Ufadhili wa Milioni 300 kwa chuo kikuu cha Sayansi na
Teknolojia cha Mwalimu Nyerere kwa ajili ya mipango ya maendeleo.Anaandika
Karoli vinsent Endelea nayo.
Akithibitisha kutoa ufadhili huo, Kaimu
mkurugenzi mkuu wa (TEA) Joel Laurent wakati wa mkutano na waandishi wa Habari amesema
Mamlaka hiyo kwa kutambua umuhimu wa sekta ya Elimu nchini wamegushwa na
kuamua kutoa pesa hizo katika kusaidia mambo mbali mbali ya maendeleo katika
chuo hicho.
Amesema sehemu kubwa ya Fedha hizo
zitakwenda katika kusaidi ujenzi wa jengo katika chuo hicho kilichopo mkoani
Mara kwa kusaidia kujenga majengo ya ofisi yatakayotumika kwenye utawala chuoni
hapo,
Wanahabari wakiwa kazini |
Pia amesema Ufadhili mwengine utakwenda katika
kusaidi walimu wa chuo hicho kwenye utungaji wa Mitahala ya kufundishia ambayo
inatazamiwa kupelekwa kwenye tume ya Vyuo Vikuu nchini TCU na kupewa hizini ili
iendelee kutumika katika kufundia chuoni hapo.
Kwa upande wake Makamu mkuu wa Chuo hicho
Profesa Domonik Kambalage ameishukuru TEA kwa msaada huo katika chuo hicho
akisema msaada huo utakuwa na chachu ya kuleta maendeleo ya chuo hicho kipya
nchini kwa kusema itasaidia kuongezeka kwa wataaalamu wa sayansi ambao ni
wachache nchini,
Aidha
Profesa kambalage pia akitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa
mchango wake aliouonyesha katika utawala wake kwa kuanzisha Chuo hicho, huku
akimtaka Rias ajae nchini kujikita katika kuanzisha viwanda.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni