MTIHANI WA DARASA LA SABA KESHO,NECTA YASEMA NENO,SOMA HAPO KUJUA
Katibu mkuu wa baraza la Mitihani nchini NECT Docta CHARLES MSONDE akizungumza na vyombo mbalimbali vya Habari leo jiji |
WANAFUNZI 775,729 wa Darasa la saba wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi nchi nzima kuanzia
kesho tarehe 09 hadi semptemba 10 mwaka huu.Anaandika KAROLI VINSENT endelea
nayo
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es
Salaam na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini NECTA DKT Chalses E Msonde wakati wa mkutano na waandishi wa
Habari ambapo amesema kati ya wanafunzi hao,Wavulana ni 361,502 sawa na
asilimia 46.6 na wasichana 414,227 sawa na asilimia 53.4.
Sanjari na hao pia nao watahiniwa
wasiona ni 76 kati yao wavulana 49 na wasichana 27,huku watahiniwa wenye uono
hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa ni 698 ambao pia wavulana ni 330 na
wasichana 368.
Msonde amesema Masomo yatakayohiniwa
ni Kiswahili,English language,Sayansi,hisabati na maarifa ya Jamii,huku Jumla
ya wanafunzi 748,514 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili,na watahiniwa
wengine 27,215 watafanya mtihani kwa lugha ya kingereza ambayo wamekuwa
wakiitumia kama somo la kufundishia.
Aidha,DK
Msonde amesema maandalizi ya mtihani huo yamekamilika kwa asilimia kubwa ikiwa
ni pamoja na kusambaza karatasi za mtihani,kusambaza kwa fomu maalum za OMR za
kujibia mtihani pamoja na Nyaraka muhimu zinazohusu mtihani .
Vilevile Dokta Msonge ametoa wito kwa kamati za mikoa na wilaya
kuhakikisha kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo ikiwa ni
pamoja na kuhakikisha kuwa mazingira ya vituo yapo salama tulivu na kuzuia
mianya yote inayoweza kusababisha udanganyifu.
Pia Baraza
hilo limesema halitasika kumchukulia hatua za kisheria mtu yoyote atakae husika
katika kufanya udanganyifu wowote utakao jitokeza.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni