MAUZO KATIKA SOKO LA HISA DSE YASHUKA TENA,SOMA HAPO KUJUA
Meneja Masoko wa DSE Patrick Mususa wakati wa mkutano na waandishi wa Habari akielezea hali ya mauzo katika soko la hisa |
MAUZO katika
soko la hisa (DSE)kwa wiki iliyopita yameshuka kwa asilimia 78 toka bilioni
29.8 hadi bilioni 4.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hayo
yamesemwa leo Jijini dare s Salaam na Meneja masoko wa DSE Patrick Mususa wakati
wa mkutano na waandishi wa habari ili kuzungumzia hali ya soko katika wiki ilioyopita
ambapo amesema mauzo katika soko hilo yamepolomoka kwa kiasi hicho inatokana na
wawekezaji kutoa hisa zao kwenye kaunta ya TBL jambo analodai ndio limechangia
mauzo hayo kushuka.
Mususa amesema Mauzo katika wiki mbili
iliyopita yalionekana kukua kutokana na Kaunta ya TBL kuongezeka mauzo lakini
kwa sasa wawekezaji walipunguza mauzo katika Kaunta hiyo na kupelekea mauzo
hayo kushuka.
Aidha,Mususa amezitaja kampuni tatu
zilizongoza kwa mauzo katika wiki iliyopita ni Benk ya CRDB ambayo imeongoza
kwa asilimia 91.11 na kufuatia na Kampuni ya Bia ya TBL nayo kwa asilimia 7.13
huku Benki ya NMB pia nayo ikiambulia asilimia 0.54.
Vilevile Mususa amewataka watanzania
kuendelea kununua hisa kupitia njia ya simu kwa kukipiga *150*36# amesema
kufanya hivyo kutawasaidi kuongezeka kwa
kipato.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni