MADUDU YA DOKTA SLAA YAZIDI FICHUKA,MCHEZO MCHAFU WABAINIKA,SOMA HAPO KUJUA
Nani
alilipia mamilioni ya ukumbi hoteli? Nani alilipia matangazo �live� katika
televisheni? Kwa nini atake makada CCM wamsaidie? Kulikoni Mwakyembe kuonekana
hotelini kabla? Iweje amkomalie Lowassana kutomgusa Magufuli? Iweje maofisa
serikali wamuandalie mkutano wake? Mkutano wake wagharimu milioni 80.
Siku moja tu baada ya
aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.
Willibrod Slaa, kutangaza kujing’atua katika siasa huku akiwashushia tuhuma
nzito viongozi mbalimbali akiwamo waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa,
maswali kadhaa yameibuka juu ya hatua ya kiongozi huyo.
Uchunguzi uliofanywa na Nipashe jana ulibaini kuwa mijadala
mbalimbali imeibuka kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na hatua hiyo ya Dk.
Slaa, huku baadhi ya viongozi aliokuwa nao katika kambi ya upinzani wakihoji
maswali kadhaa yasiyo na majibu ya wazi kuhusiana na mkutano wake wa juzi
kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkutano wa Dk. Slaa unakadiriwa kugharimu takribani shilingi
milioni 80 kulingana na takwimu zilivyokusanywa na gazeti hili hapo jana.
Katika mkutano huo aliozungumza na waandishi wa habari kwa
takriban masaa mawili, Slaa alitumia muda mwingi kumshambulia Lowassa
aliyeteuliwa na Chadema kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
akiwakilisha pia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa unaoundwa na Chadema, Chama cha
Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na National League for Democracy(NLD), James
Mbatia, ni miongoni mwa watu kadhaa walioibua maswali yasiyo na majibu ya wazi
kuhusiana na mkutano wa Dk. Slaa.
Akizungumzia Dk. Slaa kumhusisha Lowassa na kashfa ya Richmond,
Mbatia alisema hizo ni njama za kutaka kuwaondoa katika harakati kampeni za
uchaguzi mkuu na kuhoji sababu za katibu huyo wa zamani wa Chadema kujitokeza
juzi na kutoa tuhuma za kashfa hiyo ya mwaka 2008, huku akiacha baadhi ya
kashfa kubwa za ufisadi zilizotikisa nchi.
Alitaja baadhi ya kashfa ambazo zilitikisa nchi kuwa ni pamoja
na ile ya Tegeta Escrow ambayo kesi dhidi ya wahusika zilipelekwa kwenye vyombo
vya sheria, Meremeta na ile ya wizi wa mabilioni ya shilingi toka benki kuu
kupitia akaunti maalumu ya madeni ya nje (EPA).
Mbatia alishangaa Dk. Slaa kutozizungumzia kabisa kashfa hizo
kama kweli ana ajenda ya kupambana na ufisadi na kusisitiza kwamba kulikuwa na
njama ya kuwatoa kwenye ajenda ya kampeni za uchaguzi.
“Hawa wanataka kututoa kwenye reli ili tuanze kujibizana. Hatuna
haja ya kumjadili,” alisema Mbatia
Akieleza kuhusu kuwania urais kupitia Ukawa, alisema Dk. Slaa
ambaye alipitishwa na Chadema kushindana na wenzake kutoka Cuf (Prof. Lipumba)
na Dk. Kahangwa wa NCCR-Mageuzi, alikuwa akililia urais kwa kudai kuwa yeye
ndiye bora kuliko wenzake na kufanya kikao kilichomalizika usiku Juni 17 mwaka
huu kuvunjika, hivyo siyo sahihi kudai kwamba hakuwahi kuutaka urais.
Kwa mujibu wa Mbatia, Lowassa baada ya kujiuzulu akiwa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kama alithibitika kuwa na kesi ya kujibu, angeweza kushtakiwa
kwani Waziri Mkuu anapokuwa nje ya nafasi hiyo, hana kinga ya kumzuia
kushtakiwa.
Alisema Waziri Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 33, anatekeleza na kuwajibika kwa majukumu
yanayotolewa na Rais.
Pia alipinga madai ya Dk. Slaa kwamba Lowassa alisema
angekuja na wenyeviti wa mikoa na wa wilaya wa CCM wakati wa kuhamia Chadema
kuwa si ya kweli.
Alisema Dk. Slaa pamoja na wenyeviti wenza wa Ukawa akiwamo yeye
mwenyewe (Mbatia) walishiriki bega kwa bega katika mchakato wote wa
kumleta Lowassa.
Alisema Lowassa hakutoa kauli hiyo kwamba angekuja na viongozi
hao wa CCM, bali alipokuwa bado katika chama hicho hao walikuwa ni miongoni mwa
waliokuwa wanamuunga mkono.
Mbatia alisema Dk. Slaa alikuwa akililia urais na kusema kuwa
yeye ndiye bora kuliko wenzake na kufanya kikao kilichomalizika usiku
Juni 17 mwaka huu kuvunjika.
Alisema Dk. Slaa ndiye aliyesema asitangazwe kuwa mgombea
kupitia Ukawa Julai 14 mwaka huu mpaka baada ya siku saba ili kulifanya
tukio hilo kuwa la kihistoria.
Mbatia aliwataka wananchi kuepukana na hoja hizo ambazo ni
nyepesi, kwani Ukawa wanasimamia uzalendo, utu, uadilifu, umoja na uwajibikaji.
Kuhusu wito wa mdahalo kuzungumzia suala la Richmond, alisema
wapo tayari lakini hawawezi kumruhusu mgombea wao Lowassa kushiriki kwani hiyo
ni mbinu ya kuwataka watoke kwenye reli ya kuendelea na kampeni za uchaguzi
mkuu.
“Hawa wanataka kututoa kwenye reli ili tuanze kujibizana. Hatuna
haja ya kumjadili,” alisema Mbatia.
Aidha wachangiaji mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii nao
waliibua maswali kadhaa kuhusiana na hatua hiyo ya Dk. Slaa.
Wakati maswali kadhaa yakiibuka, jana kulikuwa na taarifa ambazo
Nipashe haikuweza kuzithibitisha moja kwa moja, kuhusu kutokweka kwa Dk. Slaa,
ambaye inadaiwa aliondoka nchini jana.
Hata hivyo, Nipashe lilipojaribu kumtafuta Dk. Slaa kuhusiana na
habari za kukimbilia nje, simu yake jana ilikuwa ikipokelewa na mwanamke ambaye
alikana kwamba hiyo siyo namba ya Mwanasiasa huyo.
MASWALI YALIYOIBULIWA
Baadhi ya maswali yaliyoibua kizungumkuti kuhusiana na mkutano
wa Dk. Slaa juzi ni pamoja na mlipaji wa gharama za ukumbi wenye hadhi ya juu
wa hoteli ya Serena; mlipaji wa gharama za matangazo ya moja kwa moja kwenye
televisheni tatu; kauli yake ya kutaka asaidiwe na makada wa CCM - Dk. Harrison
Mwakyembe na Samuel Sitta katika kujenga hoja za kudhihirisha kuwa Lowassa
alihusika na Richmond.
Kadhalika, maswali mengine kuhusiana na mkutano wa juzi wa Slaa
ni pamoja na swali kwamba je, bni kwa nini alimshambulia zaidi mgombea wa Ukawa,
Lowassa na kisha kutomgusa hata kidogo mgombea wa CCM, John Magufuli? Na kwamba
je, ni iweje maandalizi ya mkutano wake yahusishe baadhi ya maafisa wa serikali
waliokuwa wakitumia simu za ofisi ya umma kuwaalika waandishi wa habari?
MBOWE AJIBU KIAINA
"Safari ya Chadema ni sawa na treni, inayoanzia Dar es
Salaam kwenda Kigoma. Njiani watu wakageuka, na wakaendelea kugeuka katika
vituo vingine vya njiani. Sisi tunaendelea," alisema.
"Chadema siyo mali ya Mbowe wala kiongozi yeyote.
Anayefikiri yeye ni mkubwa hana nafasi... Kamati Kuu (CC) iliamua, na Mkutano
Mkuu uliamua vilevile kuwa Lowassa awe mgombea wa nafasi ya urais. Kama kuna
watu wana mawazo tofauti watatukuta mbele ya safari," alisema Mbowe wakati
akizungumza kwenye mkutano wa kampeni mjini Sumbawanga jana.
CHANZO: NIPASHE
Hakuna maoni
Chapisha Maoni