USHINDI WA NAPE WAIANGAMIZA CCM MKAONI LINDI,MAMIA YA WANANCHI WAHAMIA CHADEMA,SOMA HAPO KUJUA
Na KAROLI
VINSENT
ALIYEKUWA
mgombea wa Ubunge kupitia chama cha Mapinduzi CCM kwenye jimbo la Mtama
Suleiman Methew pamoja na wanachama zaidi ya elfu moja wamekiahama chama hicho
na kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
Ni baada ya kutoridhishwa na matokeo wa kura
za maoni ambayo yalimpa ushindi Katibu wa Itikadi na mwenezi wa CCM Nape
Nnauye.
Akitangaza hatua hiyo leo mkoani Lindi
na kushuhudiwa na Maelfu ya wanachama wa CCM, Methew amesema amechukua hatua
hiyo baada ya kubaini kutofanyiwa haki kwenye matokeo ya Ubunge na ndio sababu
ya kuhamia Chadema.
Amesema ushindi wa kura alioupata Nape
hakuwa kweli kwani kura elfu saba alizopata sio za kwake.
“Leo CCM sio
chama cha haki tena,yaani inauma sana mimi ndio mshindi nimepata kura elfu saba
na huyo Nape alipata kura elfu tano,lakini cha ajabu kura zangu eflu saba
kapewa Nape na elfu tano napewa mimi,jamani hapa haki ipo wapi ndani ya
CCM,bora nihame nikatafute haki sehemu nyengine na ni Chadema”amesema Methew.
Kwa upande
wake wanachama wa CCM waliohamia Chadema wamesema wamefikia hatua hiyo nao
baada ya kutofurahishwa na hatua ya uongozi wa CCM kumkombatia Nape ambaye wanadai
kuwa hakushinda kwenye kura hizo za maoni ambazo wanazidi dai kuwa Methew ndio
alishindinda na sio Nape.
Maoni 1
Gori la mkono hilo mwizi ni mwizi tu karibuni ukawa
Chapisha Maoni