HABARI KUBWA LEO.KIKWETE AWAGAWA WASANII,HALFA YAKE YAIBUA UTATA,BALAA LAMUANGUKIA RUGE WA CLAUDS,SOMA HAPO KUJUA
Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) akiwa katika hafla ya kuagwa na wasanii. Kushoto ni Katibu wa CCM, Abdulahaman Kinana. Kutoka kulia ni Waziri wa Sayansi na Tekinolojia, Januari Makamba na Mgombea wa CCM, John Magufuli picha na maktaba |
HALFA iliyoandaliwa na wanaojiita na kuitwa Wasanii
nchini kwa ajili kumuaga Rais Jakaya Kikwete imeleta mpasuko mkubwa kati ya
Wasanii wenyewe kwa wenyewe. Mtandao huu unataarifu,Anaandika KAROLI VISENT
endelea nayo
Mpasuko huo umebainika baada Umoja
wa Mashirikisho ya Sanaa nchini kuibuka na kusema Rais Kikwete ameingizwa “mkenge”
kwa kusema umoja wa wasanii uliokuwa unamuaga haupo nchini na hata usajili wake
pia haupo.
Vilevile
Umoja huo umesikitishwa na kitendo cha baadhi ya wasanii nchini kujiingiza
katika mitego ya kisiasa na kuanza kumnadi mgombea wa Urais kwa upande wa Chama
cha Mapinduzi CCM John Magufuli kwa kusema ni jambo baya ambalo litaweza
hata kuwagawa mashabiki wa sanaa nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam
na Rais wa Umoja wa Mashirikisho ya Sanaa nchini Saimon Mwakifyamba wakati wa
mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema umoja ule ulikuwa na Rais Kikwete haupo hapa nchini
kwani umoja unaotambulika na kusajiliwa sehemu mbali mbali ikiwemo baraza la
sanaa nchini BASATA ni umoja wao na sio mwengine.
“Tanzania umoja wa wasanii ndio sisi
peke,na hakuna umoja mwengine na sio ule
ambao ulikuwa na Rais Kikwete pale Mliman City, kwani ni ahadaa kubwa alizofanyiwa
Rais kwani umoja huo haujasajiliwa mahari popote,na tunashangaa sana Rais
Kikwete amekubali kwenda kwenye Halfa ya ambayo tunaiona ni ya kihuni kwani umoja ule sio wa wasanii
ni wa matapeli wachache wenye malengo ya binafsi na halfa hiyo”amesema
Mwakifyamba.
Mwakifyamba ameongeza kuwa hata wao
wanashangaa Gharama zilizotumika za
kuandaa halfa hiyo zilitoka kwa nani huku ikizingatia wasanii hao wote walikuwa
wamearikwa kama wageni wengine wanavyoenda kwenye shuhuri mbali mbali.
“Yaani tunashangaa sana maigizo ya
upotoshaji ulikuwa unasemwa na wasanii wale,tunajiuliza ni nani aliyehusika
kuandaa na kugharamia halfa hiyo huku ikizingatiwa hata wasanii wote pale
waliokuwepo pale wamepewa mwariko wa kadi kama wageni wengine na hadi sisi
tunashangaa hao wasanii wanasema wameandaa leo inakuwaje wawe wageni waalikwa
katika shuhuri wanaodai wameandaa wao”amezidi hoji.
Mwakifyamba ambaye chama chake ni
muunganiko wa mashirikisho yote ya sanaa nchini ikiwemo Shirikisho la sanaa za
ufundi Tanzania (TAFCA),Shirikisho la Firamu Tanzania(TAFF),Shirikisho la sanaa
za maonyesho nchini (TAPAF) pamoja
shirikisho la Muziki nchini (TMF) ambapo amedai walioandaa halfa hiyo walikuwa
wanaajenda ya kisiasa ya kumnadi mgombewa urais kupitia CCM John magufuli.
KUHUSU UBAGUZI KWA WASANII KWENYE HALFA HIYO.
Mwakifyamba
amesema licha ya Halfa hiyo kudaiwa ni ya wasanii lakina jambo la kushangaza
analosema Halfa hiyo imewabagua wasanii nchini kwani kunabaadhi ya wasanii
wengine hawakupewa mwariko huo huku ukizingatia wote ni wasanii nchini na
kusema ajenda ya –
Kuwabagua wasanii ilitokana na kutaka
kuwanufaisha wasanii wachache ambao walitumika na Mmiliki moja wa kituo kimoja
cha Redio nchini ambaye inadaiwa ndio alikuwa anahusika na halfa hiyo kwa
malengo yake binafsi.
KUHUSU NANI ALIYEANDAA HALFA HIYO.
Baada ya
kubanwa na waandishi wa Habari juu ya nani aliyeandaa Halfa hiyo ,ambapo
Mwakifyamba akawata waandishi wa Habari
wa mtafute aliyekuwa akisoma Risara ukumbini hapo kwa niaba ya wasanii nchini
ambaye alikuwa ni Msanii “Nikk wa pili” ,
jambo lilowachukiza waandishi wa
Habari huku wakisema yeye kama kiongozi wa hao wasanii atakuwa anamjua
aliyeandaa halfa hiyo,lakini bado Rais huyo
akisita kumtaja aliyeandaa Halfa
hiyo huku akizidi wataka Waandishi wa Habari wamtafute msanii Nikk wa pili.
RUGE WA CLAUDS AJIBU MAPIGO.
Baada ya kutambaa taarifa kwenye mitandao
ya Kijamii inayomtuhumu,Mkurugenzi wa Clauds Redio pamoja Tv Ruge Mtahaba
kwamba ndio aliyewatuma wasanii nchini kumnadi mgombea wa Urais kupitia CCM
john Magufuli pamoja na kuhusika katika kuandaa Halfa hiyo ambapo inadaiwa pia
iliwahusisha hadi viongozi wa Idara ya Usalama wa Taifa na ilikuwa na malengo
ya kumnadi Magufuli katika harakati za Urais.
Ambapo Ruge
akijibu dai moja la wasanii,wakati alipokuwa akizungumza katika kipindi power breakfast
kinachorushwa Cleuds redio amesema
anasikitika taarifa hizo kwa kusema kamwe yeye ahusiki na ahadaa hizo kwa
wasanii huku akidai Clauds redio ni taasisi kama zilivyo taasisi zengine na
haina upande wowote wa kiasiasa ikiwemo kumsapoti mgombea wa chama chochote cha
siasa.
Ruge akazidi sema kitendo cha wasanii
hao kumnadi Magufuli ni haki yao kufanya hivyo na mapenzi yao,na wala hata yeye
pamoja na Redio yake hawahusiki katika kitendo hicho.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni