MGOMO MKUBWA WA WALIMU WANUKIA,MUKOBA ASEMA LIWALO NA LIWE WAMECHOKA,SOMA HAPO KUJUA
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba |
CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT), kimeonya kuwa kitachukua hatua
madhubuti ikiwa katika kipindi cha siku 30, serikali itashindwa kulipa stahiki
zote za walimu nchini. Anaandika
Sarafina Lidwino …
(endelea).
Hatua
hiyo inatokana na serikali kupuuza madai ya walimu yaliyotaka kulipwa madeni
yao yote wanayoidai serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Rais wa CWT, Gratian Mukoba amesema,
serikali imepuuza matatizo yao na kushindwa kutoa majibu yasiyoridhisha na
yasiyo na utatuzi.
Amesema, awali chama chake na Serikali
walikubaliana kuwepo kwa muundo mpya wa utumishi kwa waalimu; muundo ambao
ulipangwa kuanza kutumika mwaka wa fedha wa 2014/2015. Mfumo ulipitishwa katika
mwaka 2013/2014.
Muundo huo mpya ulihusisha matatizo
makubwa tisa; na ambayo serikali ilikubali kuyatekeleza.
Mukoba ameeleza miundo hiyo
ambayo ilitarajiwa kutekelezwa miaka miwili iliyopita, ni pamoja na muundo mpya
wa utumishi wa waalimu; posho ya madaraka kwa wakuu wa shule; upandishaji wa
madaraja; madeni na muundo wa wakaguzi wakuu wa shule.
Anasema, serikali na CWT
walijifunga katika makubaliano yaliyotaka waalimu zaidi ya 40,000 kupanda
madaraja; kuanzia Julai mwaka huu, jambo ambalo mpaka sasa halijatekelezwa.
Mukoba amesema, walimu wanaidai
serikali zaidi ya Sh. 19 bilioni, huku walimu zaidi ya 38,000 waliopanda
madaraja wakiwa hawajalipwa mishahara.
Matatizo mengine, ni nyongeza
ndogo za mishahara na ucheleweshaji wa malipo kwa wastaafu ambapo amedai, kuna
waalimu hawajalipwa viinua mgongo tangu mwaka 2014.
Amesema, baada ya kuyapeleka matatizo
hayo serikalini hadi leo hakuna majibu ya kuridhisha kutoka kwao badala yake
wanakimbia vikao na walimu.
Anasemaa, “Agosti 19 mwaka
huu, tulipanga kuwa na kikao cha mwisho cha kujadili changamoto hizi. Lakini
serikali imekataa kukutana nasi. Sasa tumepanga kukutana Agosti 28; kikao hiki
cha sasa kitakuwa cha mwisho.”
Anasema, “…tumeshachoka kupigwa
danadana na hata wakija kikaoni wanakuja na agenda tofauti.safari hii hatutaki
ahadi tunaitaji vitendo.”
Anahoji: Kwa nini serikali inataka hadi
ishinikizwe kufanya wajibu wake kana kwamba haijui kama walitoa waraka wa
muundo mpya wa walimu?
Anasema, chama chake kitakutana baada
ya tarehe ya mwisho waliyokubaliana, ikiwa serikali haitatekeleza mwatakwa yao,
wataamua cha kufanya.
Habari hii kwanisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni