HABARI KUBWA LEO.MASIKINI DK MWAKYEMBE,SASA KUBURUZWA MAHAKAMANI,KAMPUNI ZAKE ZAMPONZA,SOMA HAPO KUJUA
Rais Jakaya Kikwete, (kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe |
WAZIRI wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, aweza
kufikishwa mahakamani, kujibu shitaka la utapeli. Anatuhumiwa kumtampeli raia
kutoka Korea, Chris Incheul Chae. Anaandika
Saed Kubenea …
(endelea).
Mwingine
awezaye kufikishwa mahakamani pamoja na Dk. Mwakyembe, ni Victor Mwambalaswa,
mbunge wa Lupa (CCM) na msemaji wa familia ya waziri huyo.
Aidha, Isaac Mwamanga, mwenyekiti wa
bodi ya kampuni ya Dk. Mwakyembe na ambaye pia ni msemaji wa familia ya
mwanasiasa huyo, naye yuko hatarini kufikishwa mahakamani katika shauri hilo.
Dk. Mwakyembe na washirika wake hao
wawili, ni miongoni mwa wamiliki wa kampuni ya kuzalisha umeme kwa njia ya
upepo ya Power Pool East Africa Limited.
Dk. Mwakyembe na kampuni yake,
wanatuhumiwa kwa utapeli, kutokana na kukiuka makubaliano ya mkataba wa
kuzalisha umeme na kampuni ya Good PM inayomilikiwa na Chris.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana
kutoka Ikulu jijini Dar es Salaam, nchini Korea, watu waliokaribu na Dk.
Mwakyembe na nyaraka mbalimbali, wamiliki wa kampuni hiyo wanatuhumiwa
kumtapeli Chris mamilioni ya shilingi kwa njia ya udanganyifu.
Chris alitoa kiasi cha dola za
Kimarekani 1.2 milioni (zaidi ya Sh. 2.6 bilioni), ili kufidia ardhi na mali
mbalimbali za wananchi wa kijiji cha Kisasida, mkoani Singida. Eneo la Kisasida
ndiko Dk. Mwakyembe na washirika wake wanakodai kukabidhiwa na serikali
kuzalisha umeme wa upepo.
Chris anamtuhumu Dk.Mwakyembe na
washirika wake kwa mambo mawili. Kwanza, fedha alizotoa hazikufikishwa kwa
wananchi wa Kisasida kama ilivyokubaliwa; na pili, Power Pool East Africa
Limited, imejifunga – kinyume cha taratibu –katika mkataba mwingine wa ubia na
Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).
Tayari Chris amemlima barua kampuni ya
Dk. Mwakyembe, akiomba arejeshewe fedha alizotoa. Barua Chris kwenda kwa Dk.
Mwakyembe imebeba Kumb. Na. PP/KOREA/22/2014. Iliandikwa tarehe 4 Februari
2014.
Katika barua hiyo, kampuni ya
Korea inasema, ilijifunga katika mkataba wa ushirikiano na Power Pool East
Africa, ili kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida.
Anasema, 22 Februari 2010, kampuni
yake ilitoa kiasi cha 316, 189.60 milioni kwa ajili ya fidia ya Ardhi katika
mradi huo.
Akiandika kwa wakurugenzi wenzake, mara
baada ya Chris kuwalima barua, Mwamanga, anasema, “deni hilo, linayaweka
mahusiano kati ya kampuni hiyo ya kigeni, katika hatari na kuchafuka mbele ya
macho ya kimataifa.”
Aidha, katika makubaliano mengine,
kampuni ya Chris ilikubaliana na Dk. Mwakyembe, kutoa kiasi cha dola za
Kimarekani 1 milioni moja (sawa na Sh. 2 bilioni).
Nyaraka zinaoyesha, kufuatia
malalamiko ya Mkorea huyo, baadhi ya wanahisa katika kampuni hiyo wenye
madaraka makubwa ya kisiasa walianza kuondoa majina yao na kuomba washikiwe
hisa zao na wanahisa wengine ili kuepuka kushitakiwa.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni