HATIMAYE YUSUF MANJI AKATWA CCM,VURUGU KUBWA ZATOKEA,SOMA HAPO KUJUA
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji picha na maktaba |
VURUGU kubwa zimetokea katika ofisi ya CCM
mkoa wa Dar es Salaam baada ya Wanachama wa chama hicho, kupinga hatua ya
uongozi wa CCM mkoani hapa kutengua ushindi wa kura ya maoni kwenye ngazi ya
Udiwani kata ya Mbagala kuu aliopata Yusuf Manji, ushindi huo kupatiwa na aliyeshika nafasi ya pili katika ngazi
hiyo Abubakari Athumani.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Wakizungumza kwa Jazba na Mtandao huu ,wanachama hao wa CCM kutoka kwenye kata hiyo iliyoko wilayani Temeke mkoani hapa wamesema wamesikitishwa na kitendo cha mwenyekiti
wa CCM mkoa Ndugu Ramadhan R. Madabida pamoja na Katibu mwenezi wa CCM mkoa
Juma Simba Gadafi wanakidai kuwa viongozi hao wamekiuka kanuni za chama kwa
kutumia ubabe kulikata jina la mgombea wao.
“Tumechoka sana na hiki chama,leo
kinaendesha kibabe sana,maana mzee Manji tumemchagua kwa kura za kishindo na
huyu ajatoa rushwa wala nini,inakuwaje wamkate jina lake bila sababu ya
msingi,na kutupa mtu wanaomtaka wao,hatukubali tunarudisha kadi zao tunahamia
UKAWA”amesema Emmanuel john mwanachama wa CCM
Mtandao
huu ulimtafuta Ndugu Ramadhan R. Madabida ambaye
ni Mwenyekiti wa CCM mkoa hapa,ili
kutaka kujua kirikoni yanatokea hayo ambapo amesema kamati ya ccm mkoa imefikia
maamuzi ya kumpokonya ushindi Yusuf Manji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya
Mpira ya Yanga ni kwa kutokana kukiuka kanuni za CCM kwa kushindwa kwake yeye
kufika mbele ya Kamati kutoa ufafanuzi juu ya tuhuma zinazomkabili.
“Huyu bwana (Manji) tumemwita kwenye
kamati aje kutuambia ameshindaje ushindi wake na ameupataje, lakini yeye alikuwa
anakaidi,tumempigia simu mara kadhaa bado apokea simu yake,basi kwa njia
hiyo,ni kinakwenda kinyume na katiba ya CCM na tumeamua kufuta ushindi wake na
kumpatia mgombea wa Pili ushindi wa kupeperusha bendera udiwani kwenye kata ya
Mbagala kuu”amesema Madiba.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni