MWANDISHI KUBENEA "KUMVUA NGUO" MASABURI,ANDAA NONDO ZA KUFA MTU,SOMA HAPO KUJUA
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, Saed Kubenea |
MWANDISHI wa habari mahiri nchini, Saed Kubenea, ameteuliwa na
Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwa mgombea
ubunge wa jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam. Anaandika Yusuf Aboud … (endelea).
Taarifa
kutoka ndani ya Chadema zinasema, Kubenea ameteuliwa kupeperusha bendera ya
Chadema kwa mwavuli wa UKAWA baada ya kushinda kura za maoni, wiki mbili
zilizopita.
Kubenea ambaye ni mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, wachapishaji wa magazeti
ya MwanaHALISI, MSETO na gazeti linatoka kwa njia ya mtandao – MwanaHALISI
Online pamoja na mtandao wa MwanaHALISI Forum, anatarajiwa kupambana na Dk.
Didas Masaburi, anayewania jimbo hilo kupitia CCM.
Akizungumza na mwandishi wa
habari wa gazeti hili, Kubenea amesema, amejitosa katika kinyang’anyiro hicho
siyo kushiriki, ila kushinda.
“Sikuja hapa kushiriki
uchaguzi. Nimekuja hapa kushinda,” ameeleza Kubenea, akiwa katika ofisi za
Chadema, jimbo la Ubungo.
Amesema, “Ninamfahamu
mshindani wangu (Masaburi). Ninajua udhaifu wake, makandokando yake na zaidi
tuhuma zinazomkabili. Muda ukifika, nitamvua nguo.”
Kubenea, mwandishi wa habari
anayeheshimika nchini, anapewa nafasi kubwa ya kushinda jimbo hilo.
chanzo ni mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni