HABARI ILIYOTIKISA JIJI,LOWASSA AVUNJA REKODI CHADEMA,SOMA HAPO KUJUA
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa alipokuwa anarudisha fomu Makao Makuu ya Chadema |
HATIMAYE Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa leo amerejesha fomu
ya kuomba uteuzi kuomba urais kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema). Anaandika
Sarafina Lidwino … (endelea).
Aidha,
katika urejeshaji wa fomu Lowassa amepata udhamini kutoka mikoa 32 ambao
amedhaminiwa na wanachama zaidi ya milioni 1.6
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
Organaizesheni na Uchaguzi, Benson Kigaila amesema, wadhamini hao wamepatikana
kutoka katika Kanda 10 na Mikoa 32 kwa nchi nzima.
“Sasa safari ya matumaini kupitia CCM
imeishia njiani,safari ya uhakika kupitia Chadema imefika na kipindi hiki
lazima kieleweke na tunaenda kuiondoa CCM madarakani asubuhi kweupe”,amesema
Kigaila.
Ameongeza kuwa wanachama kutoka
mikoa yote walikuwa wakitamani Lowassa apitie mikoa yote ili kumdhamini
kutokana na muda mchache wameamua kumdhamini kupitia njia ya simu.
Kigaila ambae pia ni Mkurugenzi wa
Kanda wa Mambo ya Uchaguzi wa chama hicho amesema wanachama wasijali chochote kwa
kuwa baada ya mkutano mkuu kumpitisha mgombea ambao unatarajia kufanyika Agosti
nne atachanja mbuga kuzunguka mikoa yote.
Nae Profesa Abdallah Safari ambae ni
Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara amesema amemshukuru Lowassa kwa kurejesha fomu
hiyo kwa kuwa baadhi ya watu walidhani angeingia mitini kwa hiyo sasa
tunajiandaa kwenda kuchukua dola.
Nae Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum
Mwalimu amesema chama tawala hawawezi kuwasambaratisha chadema na kuja kwa
Lowassa ni mpango wa mungu na nyama zote walizopanga hazitafanikiwa.
Habari hii kwa hisani ya Mwanahalisi oline
Maoni 2
Kitaele
weka tu. Siasa bwana in ngumu
Saw a
Chapisha Maoni