KUMEKUCHA SASA,MWANDISHI KUBENEA APETA UBUNGO SASA,SOMA HAPO KUJUA
Mgombea wa Ubunge Jimbo la UbungO kwa tiketi ya Chadema, Saed Kubenea (katikati) akishuhudia bonanza la mpira wa miguu Kibamba muda mfupi baada ya kushinda kura ya maoni |
MTIA nia wa Ubunge
Jimbo la ubungo kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Saed Kubenea ameibuka kidedea katika kura za maoni baada ya kuwagaragaza vibaya
wapinzani wake. Anaandika Jimmy Mfuru …
(endelea).
Katika motokeo hayo kwa kishindo Kubenea amewaacha mbali wenzake kwa
kupata kura 61 huku anaefuatia Goodluck Mollel akiambulia kura 20 na Gudat
Lehad aliyeshika mkia amepata kura nne.
Kura za Kibamba na Ubungo zimefanyika
katika ukumbini wa Happy Forest Kimara Baruti Jijini Dar es Salaam ambamo
Kubenea amejipatia ushindi huo kwa kishindo.
Hivi karibuni Kubenea aliamua kuvunja
ukimya baada ya uvumi kuenea kuwa alikuwa na nia ya kugombea ubunge katika
jimbo la Mafia mkoa wa Pwani baada ya kuchukua fomu rasmi kugombea ubunge Jimbo
Ubungo.
Kubenea ambaye ni Mwandishi Mkongwe
wa Habari za Uchunguzi amejizolea umaarufu baada ya kutunukiwa tuzo ya Shujaa
kati yetu katika kipengele cha Uwazi na Ukweli na Shirika lisilokuwa la
kiserikali la Dream Success Enterprises.
Kubenea ni nani? ni Mwanzilishi,
Mhariri Mtendaji na Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited
(HHPL), waliokuwa wakichapa gazeti la kufichua maovu la MwanaHALISI na baadaye
serikali kulifungia kwa muda usiojulikana.
Kwa sasa baada ya gazeti hilo
ambalo lillikuwa likiiumbua serikali kwa maovu yake anamiliki gazeti la
mtandaoni la MwanahalisiOnline na MwanaHALISI Forum zenye kauli mbiu ‘Uhuru
hauna mipaka’ .
Hapo awali Kubenea
alisema kutoa dukuduku na kusema “Nimeamua kugombea
jimbo la Ubungo ninaamini ni demokrasia na ni haki yangu kufanya hivyo kama
mtanzania” huku akizungumza kwa kujiamini kwa kurejea kauli ya baba waTaifa,
Mwl. Nyerere aliyesema “wananchi wana hitaji mabadiliko, wasipoyapata ndani CCM
watayatafuta nje ya CCM”.
Kwa vile wananchi
wameshindwa kupata mabadiliko ndani ya CCM , kubenea amesema ameamua kugombea
nafasi hiyo kupitia tiketi ya Chadema, chama makini, iliaweze kuwa sehemuya
Bunge ya kutunga sheria na kuisimamia serikali kwa maslahi mapana ya watanzania
na ustawi wa nchi kwa ujumla.
Aidha, alisema kuwa
kwa miaka mingi amekuwa akipambana na ukandamizaji wa serikali kwa njia ya
kalamu kupitia magazeti yake, “nimekuwa nikifanya shughuli za Bunge nje ya
Bunge” amesema sasa kuna umuhimu wa kuwa mbunge halisi na ninaamini nitakuwa
mbunge mzuri na mwenye weledi kuitumikia nchi yangu kwani ninauzoefu mkubwa wa
uendeshaji wa bunge lenyewe, siendi bungeni kujifunza kanuni za bunge kwani
ninajua hata milango ya kutokea, Kubenea alisisitiza huku akijiamini.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni