BREAKING NEWS,SAKATA LA DOKTA SLAA TENA LACHUKUA SURA NYENGINE,SOMA HAPO KUJUA
HABARI
zillizotufikia mda huu zinasema Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Dokta Wilbroad Slaa ameshindwa kutokea tena kwenye vikao muhimu vya
maamuzi vya chama hicho,
Baada ya leo kutotokea tena kwenye mkutano mkuu
wa Baraza kuu la uongozi la Chama hicho unnaofanyika mda huu kwenye hoteli moja hapa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwandishi wetu KAROLI VINSENT aliyekuwepo ndani mkutano huo
mkubwa, anasema viongozi wote wa Taifa wa chama hicho walikuwepo isipokuwa Dokta
slaa peke yake.
Ambapo Viongozi ambao hapo awali walitazamiwa
wasingekuwepo kwenye mkutano huo,ni Naibu katibu Mkuu bara John Mnyika, pamoja
na Kada wa wa chama hicho Profesa baregu ambapo katika hali ya kushangaza wote kwa pamoja
walikuwepo mkutanoni hapo pasipo kuwepo Dokta Slaa.
MBOWE AOKOA
JAHAZI
Akiwatoa
hofu wajumbe hao, Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho ,Freeman Mbowe ambapo amesema katika
hatua zote za kumruhusu lowassa ahamie kwenye chama hicho Dokta Slaa alikuwepo na alikubali maamuzi hayo, ila wanashangaa katika hatua za
mwisho Katibu huyo kuaanza kuwa tofauti nao.
“Mjue wakati lowassa kabla ya kuja kwake, tulifanya vikao vyote muhimu na kamati kuu huku Slaa huyo hakiwepo ila dakika za mwisho ndio
mwenzetu huyu akatofautiana nasi”
Ameendelea
kusema kila siku chama hicho kinafanya vikao ili kuhakikisha kuwa
wanamaliza tofauti na Dokta Slaa.
“Kila siku
tunafanya kikao na jana hata mimi nimefanya naye kikao naye,mimi nikamwambia
wazi kwamba basi akae likizo harafu na sisi tutaendelea na mapinduzi yetu na yeye apumzike na rikizo yake na akiwa teyari aje tuendelee na mapambano”ameendelea
kasema Mbowe.
Mbowe ambaye
ni Mbunge wa Jimbo la Hai akawataka wajumbe wa kutano huo wachague chama hicho kuwa chama hicho kibaki kikitafuta suluhu na Dokta Slaa au waendelee na mapambano na kuiondoa CCM
madarakani ambapo wajumbe hao waliitikia kusema -
“Ndio
tuendelee na mapambano”
Endelea
kufuatilia mtandao huu,utapata taarifa kamili
Endelea kufuatilia mtandao huu,utapata
taarifa kamili.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni