HABARI KUBWA LEO SIRI YA DOKTA SLAA NA MGOGORO WAKE CHADEMA HII HAPA,SOMA HAPO KUJUA
pichani ni Benard Membe |
WAZIRI wa
Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Benard Membe imebanainika kuwa ndiye
anayehusika katika kupandikiza mgogoro kati ya Katibu wa Chama cha demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA),Dokta Wilbroad Slaa na Chama chake.(Mtandao huu
umebaini).Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Dokta Slaa kwa sasa inatajwa kuwa na
mgogoro mkubwa na chama chake kwa kile kinachodaiwa ni “kutorizika” na ujio wa
Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa na kupewa nafasi ya kuwania Urais ndani ya
Chadema.
Taarifa za kuaminika ambazo
Fullhabari.blog imezipata zinasema mgogoro huo unapewa nguvu kubwa na Benard
Membe kwa madai ya kufanya kila liwezekano Lowassa akose Urais nchini.
Membe ambaye alikuwa ni miongoni mwa
makada wa CCM waliokosa nafasi ya Urais kupitia chama hicho baada ya kuangushwa
kwenye kura za wajumbe wa Halmashauri kuu NEC,
Taarifa hiyo inasema, Membe
anashirikiana na viongozi mbali mbali wa Idara ya Usalama wa Taifa wakitumia
njia ya “kumrubuni” mke wa Dokta Slaa, Josephine Mshumbuzi ili kuhakikisha anamzuia mumewe
asibaki chadema.
“Ujue Membe anahasira sana na Lowassa maana
anajua hata kura zilizopigwa NEC za kumkataa yeye zilitokana kwa kiasi kikubwa
na Lowassa,sasa ameamua kujitosa kwenye mgogoro huu na kuhakikisha kila aina ya
njia inatumika,kuipunguza nguvu Chadema kuhakikisha chama hichi kinakosa nguvu
na kupelekea hadi lowassa kukosa urais”
“Na malengo hayo ni kwamba wanajua Dokta
Slaa akiondoka Chadema,lazima chama hicho kitakosa nguvu na kushindwa vibaya
sana kwenye uchaguzi mkuu”amesema mtoa taarifa wa Fullhabari.blogs.
Amesema njia inayotumika ya kumrubuni Mke wa
Slaa ni ya aina ya kipekee ikiwemo kumwandalia donge nono la fedha endapo akifanikisha mpango wa
kumshawishi Slaa “kuitosa” chadema.
Taarifa zinasema kwa sasa Mama Mshumbuzi
ameanza kutumia njia mbali mbali ikiwemo
ya kuingilia mawasiliano ya Dokta Slaa kwenye Mitandao ya kijamii ka kuandika
vitu vitakavyo wachanganya wananchi,
“Huyu mama
ni mtu wa ajabu sana,kwakuwa anazijua (passwed) za mumewe kwenye mitandao huu
ya kijamii sasa amekuwa akiingia na kuandika
mambo ya ajabu sana,na kusema kweli anakishusha nguvu chama”
MBOWE AJIBU MAPIGO
Akiwatoa hofu wajumbe
Baraza la viongozi wa chadema leo Jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Taifa wa
chama hicho ,Freeman Mbowe ambapo amesema katika hatua zote za kumruhusu
lowassa ahamie kwenye chama hicho Dokta Slaa alikuwepo na alikubali maamuzi
hayo, ila wanashangaa katika hatua za mwisho Katibu huyo kuaanza kuwa
tofauti nao.
“Mjue wakati lowassa kabla ya kuja kwake,
tulifanya vikao vyote muhimu na kamati kuu huku Slaa huyo hakiwepo ila
dakika za mwisho ndio mwenzetu huyu akatofautiana nasi”
Ameendelea kusema kila siku chama
hicho kinafanya vikao ili kuhakikisha kuwa wanamaliza tofauti na Dokta
Slaa.
“Kila siku tunafanya kikao na jana hata
mimi nimefanya naye kikao naye,mimi nikamwambia wazi kwamba basi akae likizo
harafu na sisi tutaendelea na mapinduzi yetu na yeye apumzike na rikizo
yake na akiwa teyari aje tuendelee na mapambano”ameendelea kasema Mbowe.
Mbowe ambaye ni Mbunge wa
Jimbo la Hai akawataka wajumbe wa kutano huo wachague chama hicho kuwa chama
hicho kibaki kikitafuta suluhu na Dokta Slaa au waendelee na mapambano na
kuiondoa CCM madarakani ambapo wajumbe hao waliitikia na kusema -
“Ndio tuendelee na mapambano”
Hakuna maoni
Chapisha Maoni