Zinazobamba

HABARI KUBWA LEO,NI LOWASSA NI LOWASSA KILA KONA,SAFARI YAKE YA IKULU YAANZA SASA,SOMA HAPO KUJUA

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akikabidhiwa fomu ya kuwania Urais na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akikabidhiwa fomu ya kuwania Urais na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

MWANACHAMA mpya wa Chadema, Edward Lowassa, ameanza tena safari yake ya kuelekea Ikulu. Leo (Alhamisi) amechukua fomu ya kuwania urais, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaandika Hamis Mguta, DSJ … (endelea).
          Lowassa alichukua uamuzi huo wa kihistoria majira ya saa 6 mchana, makao makuu ya Chadema, Ufipa, jijini Dar es Salaam. Alilakiwa na maelfu ya wanachama, washabiki na wafuasi wa kiongozi huyo.
        “Tumeanza safari mpya ya matumaini na kuelekea ushindi. Sina cha kuwalipa, ispokuwa ninawaahidi kuwa nitawafanyia kazi itakayoleta ushindi,” amesema Lowassa mara baada ya kukabidhiwa fomu.
         Lowassa, mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi mkubwa nchini, alijiengua Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jumanne iliyopita na kujiunga na Chadema, ambako anatarajiwa kugombea urais kupitia Muungano wa UKAWA.
             Taarifa zinasema, ujio wa Lowassa ndani ya Chadema, utaingiza wenyeviti wa mikoa 22 kati ya 32 na wilaya 80 kutoka CCM.
           Tayari aliyekuwa mkurugenzi wa uchaguzi wa CCM, Marson Chizii, Balozi Bandora na aliyekuwa naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Godluck Ole-Medeye, wametangaza kujiunga na Chadema.

FAIDI PICHA ZOTE HIZO


Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi mbalimbali wa chama cha CHADEMA waliofika kumshuhudia akiwa sambamba na Mkewe Mama Regina akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam. 
 Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa akiwa sambamba na Mkewe Mama Reginal akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam.  
Rabsha za hapa na pale zilikuwepo kama uonavyo pichani wakati Mh.Lowassa akiwasili Makao Makuu ya CHADEMA  yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho.
 Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi mbalimbali wa chama cha CHADEMA waliofika kumshuhudia akiwa sambamba na Mkewe Mama Regina akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam. 
 Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa akiwa sambamba na Mkewe Mama Reginal akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam. 
 Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa akisalimiana na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu wakati alipofika kwenye Makao Makuu ya Chama hicho tayari kwa kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia Chama hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe.
 Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Salum Mwalim akizungumza jambo katika kikao kifupi ndani ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, kwenye makao Makuu ya Chama hicho, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
 Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe akisisitiza jambo kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mwanahabari, Said Kubenea wakati akiwasili kwenye Makao Makuu ya CHADEMA, Kinondoni jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe na wa pili kushoto ni Mke wa Mh. Lowassa, Mama Regina Lowassa.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA - Zanzibar, Salum Mwalim.
 Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu akitoa ufafanuzi wa kisheria wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi fomu ya kuwania Urais wa Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa.
 Sehemu ya Viongozi mbali mbali wa CHADEMA wakiwa kwenye shughuli hiyo.
 Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu akifafanua jambo.
 Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe akimkabidhi Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kupia Chama hicho, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akionyesha Fomu ya Kuwania Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, leo kwenye Makao Makuu ya Chama hicho, Kinondoni Jijini Dar.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fedha za kuchukulia Fomu ya Kuwania Urais kutoka kwa WamaCHADEMA waliojitolea kumlipia.
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza jambo na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu. 
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza machache mara baada ya kuchukua Fomu ya Kuwania Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
 People'ssssss..........
 Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe akizungumza machache.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akionyesha Fomu kwa wanaCHADEMA waliofurika kwa wingi kwenye Makao Makuu ya CHADEMA leo. Wengine pichani toka kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe, Mama Regina Lowassa na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA-Zanzibar, Salum Mwalim.


















Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline

Hakuna maoni