MASKINI SPIKA NDUGAI SASA KUFIKISHWA MAHAKAMANI,UWENDA AKAISHIA KUJUTA,SOMA HAPO KUJUA
JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma limesema kwamba limeisha
kamilisha jalada la kumshitaki Naibu Spika Job Ndugai kutokana na kumpiga
mgombea mwenzake wa CCM, Dk. Joseph Chilongani.Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Akizungumza na chanzo chagu Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime amesema kwamba jeshi hilo limechukua uamuzi
huo kutokana na mlalamikaji kutoa taarifa katika kituo cha polisi na kuandika
maeelezo ya kupigwa kwake.
Amesema baada ya kupigwa Dk .Chilongani
alienda katika kituo cha polisi wilayani Mpwapwa na kutoaa maelezo na kupatiwa
PF3 kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Misime amesema jeshi la polisi liliweza
kumkamata Ndugai lakini alijidhamini kwa mali yake mwenyewe na kutokana na hali
hiyo jeshi la polisi limeisha kamilisha uandaaji wa jalada la mashitaka ambalo
litapelekwa kwa mwana sheria wa serikali kwa ajili ya kwenda mahakamani.
“Jeshi la polisi limeisha fanya taratibu
zake baada ya mlalamikaji kufika katika kituo cha polisi na alipatiwa PF3 kwa
ajili ya matibabu ,na baada ya hapo alitafutwa mtuhumiwa abaye ni Job Ndugai
nayealitoa maelezo yake na kujidhamini kwa mali zake.
“Kutokana hali hiyo jeshi la polisi
limeweza kukamilisha jarada la mshitaka ambalo litaperekwa kwa mwana sheria wa
serikali ili hatua nyingine za kisheria kufuatia ziweze kukamilika sisi
tumeisha kamilisha taratibu zote, tunasubiri ripoti ya daktari ambaye alimtibu
Dk. Chilongani ili tuwezekuambatanisha na tumkabidhi mwana sheria wa serikali
ili awezekufanya majukumu yake,” amesema Misime.
Mbali na hilo Misime amesema jeshi la
polisi linafanya kazi zake kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu na
halitaweza kumuonea mtu yeyote kulitokana na hela zake, umaarufu na badala yake
kazi itafanyika kwa ueledi mkubwa.
Kuandaliwa kwa jarada hilo kunatokana
na Job Ndugai kumshabulia mgombea mwenzake Dk.Chilongani ambaye alipigwa na
kuzimia hadi kufikia hatua ya kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Kongwa.
Hata hivyo wagombea wenzake na
Ndugai wametishi kujiengua CCM aiwapo kamati ya nidhamu ya CCM taifa
haitamchukulia hatua kali za kinidhamu Job Ndugai kutokana navitendo vya
uvunjaji wa sheria na kanuni.
Akizungumza na waandishi wa habari
mmoja wa wagombea Samuel Chimani amesema Ndugai amekuwa kinala mkubwa wa
uvunjifu wa maadili ndani ya chama.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni