Zinazobamba

HABARI KUBWA LEO,CCM YAMUIBUKIA LOWASSA,NAPE ATIA MCHANGA PILAU LAKE UKAWA,SOMA HAPO KUJUA

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
 picha  na Maktba


Ndugu wananchama wa Chama cha Mapinduzi-CCM ni wiki mbili tangu tulipo maliza mchakato ndani ya chama kumpata mgombea wa Urais hapo Octoba 25, 2015. 

         Kwa mara ya kwanza wananchama 41 waliomba kuteuliwa na chama. Hii inaonyesha kwamba demokrasia imekuwa ndani ya chama. Kati ya wanachama wa CCM waliochukua fomu alikuwa ni mheshimiwa waziri mkuu mstaafu Ndugu Edward Lowasa.
       Utaratibu wa chama ulifuatwa ili kumpata mgombea ikiwa ni pamoja kamati ya maadili, kamati kuu na halmashauri kuu ya taifa na mkutano mkuu.
            Katika mchakato pia chama kilitumia idara mbalimbali kama usalama wa taifa, takukuru na tume ya maadili ya umma kupata taarifa mbalimbali kuhusu wagombea hasa za uadirifu, usalama wan nchi na kadhalika.

           Baada ya mchakato kumalizika baadhi ya wagombea na wanachama hawakuridhika na matokea, katika chama kikubwa kama CCM haizekani wanachama wote wakaridhika na maamzi. Ndugu wanachama na watanzania tunaomba kuelewa kuwa kumpata kiongozi mkubwa wa nchi kama Rais siyo kazi rahisi.
      Baadhi ya wanachama ambao hawakuridhika na maamzi ya chama ni Ndugu Edward Lowasa, amekuwa akizungumza nje ya chama kuhusu kutotendewa haki na baade kuhama chama na kujiunga na chamacha demokrasia na maendeleo-CHADEMA.
         Kwa nini Ndugu Lowasa hakuteuliwa kuwa mgombea wa CCM?


          Ndugu wanachama na watanzania, Mheshimiwa Lowasa alijenga hisia na kuamini kuwa ndani ya CCM wagombea wote walistahili kuenguliwa isipokuwa yeye. Hii siyo demokrasia, baada ya kupitia repoti mbalimbali Ndugu LOWASA alienguliwa kwa sababu zifuatazo:-

    1. Kukiuka taratibu za chama kwaani alionekana kufanya kampeni badala ya kutafuta wadhamini

      2. Kutoa rushwa kwa wanachama mbalimbali hivyo kukigawa chama na kama angepishwa kuwa mgombea CCM ilikuwa katika hatari ya kuwekewa pingamizi mahakamani lakini pia angeweka watu wake kwenye utawala kuwalipa fadhira.

         3. Edward Lowasa aliwahonga wajumbe katika uchaguzi wa wajumbe NEC uliofanyika miaka iliyopita ili kupata watu wake ndani ya NEC.

         4. Kuanza kampeni kabla ya wakati, alikuwa akisafirisha watu mbalimbali na kuwalipa fedha nyingi kisha kutoa taarifa kuwa walikuwa wakimtaka kugombea Urais, hii ni hadaa na hatari kwa chama.
        5. Kuwa na kashfa nyingi za ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi ya umma akiwa waziri

        6. Kusemwa semwa kuhusika kuhusika na tuhuma za kutumia watu kudhuru baadhi ya watanzania na viongozi, hili lipo kwenye vyombo vya dola kwa uchunguzi, uchunguzi ukikamilika sheria itachukua mkondo wake.
        7. Utajiri na mali usiokuwa na maelezo alizipataje kama vile kumiliki majumba nje ya nchi kama uingereza, singapole na nk

        Mwisho chama kimesikitishwa sana na kauli kuwa amekuwa akionewa na kusingiziwa kuwa alihusika na kashfa ya RICHMOND, ndugu wanachama kashfa ya RICHMOND ilianzia bungeni,
CCM haikuhusika na kumwondoa kwenye uwaziri mkuu, lakini kwa kuwa imekuwa inajengeka kuwa alionewa tunaviomba vyombo vya sheria kulipeleka jambo hili mahakamani ili kuondoa dhana inayojengeka kuwa serikalia ya CCM inaonea wanachama wake.

 Doa linalotakwa kujengeka litapatiwa ufumbuzi na iwapo inathibitika kulikuwa na njama binafsi wote waliohusika kulidanganya bunge watachukuliwa hatua na chama lakini pia sheria itachukua mkondo wake

Imetolewa na :-

Nape M.Nnauye

KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA

ITIKADI NA UENEZI

Maoni 3

mlela alisema ...

Siasa tuuuu

mlela alisema ...

Mtatapatapa

Unknown alisema ...


3. Edward Lowasa aliwahonga wajumbe katika uchaguzi wa wajumbe NEC uliofanyika miaka iliyopita ili kupata watu wake ndani ya NEC

TUNAOMBA MAJINA YA WALIO ONGWA NA MSH. LOWASSA,

UTAKUWA SI HAKI KUMTAJA ALIYEONGA NA KUTOWATAJA WALIONGWA,