Zinazobamba

TANESCO YAJIVUNIA MAKUBWA CHINI YA UTAWALA WA KIKWETE,SOMA HAPO KUJUA



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme (Tanesco),Mhandisi Felchesmi Mramba akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafanikio ya miaka 10 ya shirika hilo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam.



Sehemu ya waandishi wa habari wakifatilia taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco,hayupo pichani katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

SHIRIKA la Umeme (Tanesco) limesema kuwa limepata mafanikio katika kipindi cha miaka 10 na kuwa  ziada ya umeme kutokana na utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.

            Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kuwa walipoanza 2004 walikuwa na Megawati 891 na kufikia 2014 wamekuwa na Megawati 1501.

          Amesema mahitaji ya umeme kwa sasa nchini ni Megawati 934 hali hiyo inaonyesha kuwa kutokana na miradi mbalimbali kutakuwa na ziada kubwa ya umeme na kuongeza uchumi katika nyanja mbalimbali

          Mramba amesema kuwa hivi karibuni wataunganisha Megawati 150 za Kinyerezi namba moja katika Gridi ya Taifa na  katika kuunganisha huko kutakuwa na tatizo la umeme katika maeneo mbalimbali.
            Amesema tatizo la umeme la kuunganisha litafanyika usiku Agosti 31 na wananchi wametakiwa kununua umeme katika siku mbili hizi ili waweze kuondokana na tatizo la umeme na hakuna manunuzi yatakafanyika kwa Agosti 1 mwaka huu
            Amesema  kuna mazungumzo na Serikali ya China katika mradi wa umeme wa Kilowati 400 kwa Chalinze pamoja na kilowati 400 zingine kutoka Chalinze hadi Segera mkoani Tanga. 
habari hii kwahisani ya michuzi,blogs

Hakuna maoni