CHAMA CHA ADC YAKISHUKIA CHADEMA KUHUSU LOWASSA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mwenyekiti wa chama cha ADC Said Miraji akizungumza na waandishi wa Habari mda huu Jijini Dar es Salaam |
SIKU chache
kupita baada ya Waziri mkuu wa Zamani Edward Lowassa kukihama chama chake cha
awali cha Mapinduzi CCM na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema,navyo vyama vingine vya upinzania vimekishukia Chadema na kusema kimeua
upinzani nchini.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akizungumza na waandishi wa Habari mda
huu jiijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha ADC Said Miraji wakati alipokuwa
anazungumzia suala la Lowassa kuhamia Chadema ambapo teyari ameshachukua fomu
ya Kugombani Urais kupitia Chadema.
Chadema ambao umeunda Vyama vya
upinzani vya kutetea katiba ya Wananchi UKAWA,ambapo Miradi amesema kwa sasa
vyama vya upinzania vimejishusha hazi kwa watanzania.
“Kitendo hiki kimezidi kujidhililisha
kuwa vyama vya upinzani tunavyozungumza vitu basi vinavyokuwa ni vya uongo,kwasababu
Katibu mkuu wa chadema Dakta Slaa alihaminisha umma kwamba lowassa ni miongoni
mwa mafisadi papa”
“harafu leo wamemkaribisha kwenye chama
chao na kumpa nafasi ya Urais,sasa leo watanzania watatuona sisi wapinzani ni
waongo maana yale aliyoyasema Slaa pale mwembe yanga ni yaongo au?”amehoji
Miraji.
Miraji ameongeza kuwa kitendo cha
chadema kumsimisha lowassa kunazidi leta mpasuka kwa wananchama waliokijenga
chama hicho kwa zaidi ya miaka 20.
“Inakuwaje mtu ahamie leo na leo hiyo
apewe uongozi tena wa juu,maana ndani ya chama hicho kuna makada waliokijenga
chadema toka 1992 lakini leo hao hao hwapewei nafasi ya kugombani urais badala yake
leo unawatupa unampa mtu aliyekuja leo kisa anaumaarufu wa watu,je hivi
unategemea wanancha wengine hawatakubali”ameongeza.
Aidha Miraji amekihatarisha Chadema
kuacha tabia ya kutegemea kuwachukua wabunge na madiwani kutoka CCM na kuwapa
uongozi kwa kusema suala hilo litaweza kukivuruga chama hicho kwa madai ya kuwa
CCM wamepandikiza watu wake kuja kumaliza upinzani nchini.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni