BILIONI 10 ZA LOWASA ZAANGAMIZA UKAWA, CHADEMA SASA HAKUKALIKI, WENGI WASHIKWA NA BUTWAA
Hali ya kisiasa nchini inazidi kuwa tete, kufuatia hatua ya
Chadema kukiuza Chama hicho kwa Waziri Mkuu aliyelazimishwa kujiuzulu
kwa kashfa ya ufisadi wa kampuni ya Richmond, Edward Lowassa.
Makubaliano ya Chadema kumuuzia Lowassa Chama hicho
yamefanywa Jumapili iliyopita kati ya Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman
Mbowe na Lowassa ambapo Lowassa alikubali kutoa shilingi Bilioni kumi
taslim ili aweze kutimiza safari yake ya matumaini ya kugombea Urais kwa
tiketi ya Chama hicho, baada ya jina lake kukatwa na CCM, kwasababu ya
makandokando ya Ufisadi yanayomkabili.
Hatua ya Mbowe kukiuza Chama hicho kwa Lowassa imemkera mno
Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Wilibrod Slaa. Sababu kubwa ya Dk. Slaa
kupinga Lowassa kupokelewa Chadema na kuuziwa chama hicho ili aweze
kugombea Urais, ni imani kubwa aliyonayo kwamba Lowassa ni Fisadi mkubwa
ambaye alistahili kuwa Gerezani au kunyongwa, badala ya kupewa heshima
ya kugombea Urais katika Chama hicho.
"Kama Lowassa huyu huyu amekatwa na CCM kutokana na ufisadi
wake, vipi leo aonekane ni msafi ndani ya Chadema?!", amenukuliwa
akihoji na kulalamika Dk. Slaa.
Kutokana na kinyongo hicho alichonacho Dk. Slaa dhidi ya
Mwenyekiti wake Mbowe kwa kukiuza chama hicho kwa Lowassa, duru za
kisiasa nchini zimebainisha kuwa Dk. Slaa mapema wiki ijayo atafanya
maamuzi magumu ya kukihama chama hicho Ili kuachana kabisa na siasa au
ikibidi kurejea katika chama chake cha zamani cha CCM.
"Kamwe siwezi kukaa meza moja na Fisadi Lowassa ambaye
nilimtangaza kwa kinywa changu mwenyewe katika list of shame pale
Mwembeyanga. Ni afadhali hata niachane kabisa na Siasa na ikibidi nirudi
katika kazi yangu ya Kanisa kuliko kukaa meza moja na Mafisadi",
amenukuliwa akiapa kwa uchungu mkubwa Dk. Slaa ambaye anasifika mno kwa
ukali wake wa mapambano dhidi ya Mafisadi hapa nchini.
MWANAHARISI FORUM
Maoni 1
Lowasa ni mwadilifu ata magufuli pia. Kati yao wote wanasifa za urais
Chapisha Maoni