Zinazobamba

CUF YAWASIHII WATANZANIA SOMA HAPO KUJUA


CHAMA cha Wananchi (CUF) wilaya ya Kondoa kimewataka wananchi wa Wilaya hiyo 
kufanya mageuzi ya uongozi kwa kuchagua wagombea wa vyama vya upinzani 
ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kuleta maendeleo.

           Hayo yalisemwa na Katibu wa CUF wilaya ya Kondoa, Jafari Ganga alipokuwa 
akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya CUF Dar es Salaam 
jana.

         Alisema kwa miaka mingi wilaya ya Kondoa imekuwa ikitawaliwa na Chama cha 
Mapinduzi (CCM)katikangazi mbalimbaliza viongozi wa juu wakiwemo wabunge
ambao kila mara wanatoka chama tawala.

         Ganga alisema kuendelea kudidimia kwa uchumi wa wilaya hiyo kutokana na  uongozi ambao hausimamii ipasavyo maendeleo ya uchumi, hivyo baada ya  kuona hivyo CUF ilianza kuonesha njia kwa kusimamia mambo mbalimbali ya 
kiuchumi yaliyofanya chama kukubalika.

Alisema mpaka sasa katika kata zote 29 za wilaya ya Kondoa zimesimika matawi ya
chama hicho na wanatarajia kutwaa viti vya madiwani na Ubunge katika 
majimbo mawili ya Kondoa Vijijini na Kondoa.

"CUF imeamka inayo matawi 160 katika katika Kata zote 29 za wilaya ya  Kondoa, tumejiandaa kutwaa viti vya madiwani na wabunge" alisema Bw.  Ganga.

Alizitaja Kata hizo kuwa ni Kondoa mjini, Chemchem, Kilimani, Kingale, Kolo, Bolisa, Serya, Suruke, Hondomairo, Changaa, Thawi, Sowera, 
Kikilo,Salanka, Bereko, Kisese,Kikore, Itololo,Masange, Mnenia, Itaswi, 
Bumbuta, Pahi, Kinyasi,Keikei, Busi, Haubi, Kwa Delo, na Kalamba.


Wilaya ya Kondoa umegawanywa na kuwa majimbo mawili ya Kondoa na Kondoa 
Vijijini pia kuna Jimbo la Chemba ambalo Mbunge wake aliyemaliza muda 
wake ni Juma Nkamia.

Habari hii kwahisani ya michuzi.blogs

Hakuna maoni