Hata mimi nimechukua fomu ya Urais :Naibu meya wa Manispaa ya Iringa ambae ni diwani wa kata ya Ilala Bw Gervas Ndaki akifurahia kushika mkoba wenye fomu ya CCM ya kuomba kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,fomu ya Monica Mbega baada ya mgombea huyo kufika mjini Iringa kusaka wadhamini 30
Na Matukiodaima Blog
WAKATI mbio za makada wa chama cha mapinduzi (CCM) waliotia nia ya kuomba kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi za urais zikiendelea kushika kasi kwa kila mgombea kutumia mbinu yake ya kuwafikia wana CCM kuomba udhamini , aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini Monica Mbega leo ameingia wilaya ya Iringa mjini mkoani hapa kuomba udhamini na kupata wajumbe 33 huku akiwataka watanzania kutoaminishwa na mbwembwe za watia nia wenzake wanazofanya mikoani na kuwa yeye ndie Rais wa awamu ya tano baada ya Dr Jakaya Kikwete na kuwataka watia nia wenzake wamuunge mkono.
Mbega ambae alilazimika kusubiri wajumbe 30 wa kumdhamni kwa zaidi ya masaa manne katika ofisi ya CCM wilaya ya Iringa mjini alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanahabari juu ya safari yake hiyo ya kutaka kwenda Ikulu na kudai kuwa amelazimika kuzuia viongozi wa CCM wilaya ya Iringa kutomuandalia mbwembwe zozote wala wapambe wa kumshangilia wakati wa safari yake hiyo ya kutafuta wadhamini.
Alisema kuwa kuwa anamtegemea Mungu zaidi katika safari yake hiyo ya kwenda Ikulu na ndio maana hakupenda kuweka makisio ya gharama za safari nzima ya mchakato huo wa kuelekea kupokea kijiti kwa Rais Dr Kikwete na hivyo ndio sababu ya yeye kuzunguka bila ya mpambe zaidi ya dereva anayemuendesha pekee.
" Naomba niwaelezeni wazi kuwa sina mgombea wa kumuunga mkono kati ya wote waliojitokeza zaidi ya 30 kwani naamini kuwa namba moja kati ya wote hao waliojitokeza ni Monica Ngenzi Mbega ninasema hivyo kwa kuwa nchi ya sasa inahitaji mwamanke kuongoza kwani mwenye kuweza kuvunja makundi ni mwanamke sio mwanaume tena .....mwanamke ni mwepesi wa kusamehe sio mtu wa makundi hivyo kama hivyo ndivyo ukitanguliza upendo makundi hayatakuwepo ila wapo wenye visasi vya kutoka mwaka 2005 ila sio mimi ....mimi nimetanguliza upendo zaidi....mimi ni mama nitaiunganisha nchi na changamoto inayomkabili Rais wa awamu ya tano ni jinsi na kuiunganisha nchi na mimi ndie pekee wa kuunganisha nchi hii"
Alisema kuwa iwapo watanzania wataunganishwa kuwa wamoja kuna uwezekano wa nchi kuachana na utegemezi na hivyo wananchi wake kuwa wamoja na kuweza kushiriki kujiletea maendeleo yao chini ya rais wao Mbega .
Hivyo alisema kuwa iwapo chama chake kitamteua na watanzania wakamchagua na kuingia Ikulu wategemee Tanzania mpya yenye amani ,upendo na mshikamano na uchumi bora kwa kila mtanzania kuongeza pato binafsi .
Mbega alisema kuwa tayari Rais wa nchi Dr Kikwete amepata kuueleza umma kuwa misaada ambayo nchi inapata kutoka kwa wahisani mingine ina masharti magumu na ndio maana ya baadhi ya miradi kushindwa kukamilika kwa wakati na kuwa iwapo yeye ataingia Ikulu atajaribu kukwepa misaada hiyo na kulijenga Taifa linalojitegemea lenyewe ili kuto kuwa na miradi isiyo kamilika kutokana na masharti magumu ya wahisani .
Alisema kuwa kikubwa kilichomsukuma kuchukua fomu ya kutia nia kuomba kuteuliwa kuwania Urais ni uzalendo wake katika Taifa wenye shauku la kuliongoza Taifa la Tanzania kama mwanamke wa kwanza toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 bila ya kuongozwa na mwanamke na kudai kuwa hakuna mgombea wa CCM ambae anajambo lake binafsi la kufanya zaidi ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.
"Falsafa yangu ni kusahihisha changamoto zinazoonekana katika kutekeleza ilani hatujaweza kufanikiwa hili ....mheshimiwa Rais Dr Kikwete tunaona jinsi anavyotekeleza ilani katika sekta mbali mbali ila utasikia katika vikao vya kamati kuu wakati akitoa taarifa ya utekelezaji kuwa kuna changamoto mbali mbali ambazo zimekwamisha utekelezaji wa ilani hivyo mimi nitaanzia kutekeleza changamoto kwanza .....kwani bajeti inayotengwa ndio inapaswa kusimamiwa kwanza mwelekeo mzima wa serikali yangu ni kuona tunapata Taifa la watu wanaojitegemea wenyewe"
Katika hatua nyingine Mbega ambae aliangushwa nafasi ya ubunge mwaka 2010 na mbunge Peter Msigwa (Chadema) alisema kuwa bado ana nguvu ya kurudi kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini na kumshinda mbunge wa sasa mchungaji Msigwa kwani bado nguvu za kurejesha jimbo hilo CCM anazo japo hana mpango wa ubunge zaidi ya kutimiza dhamira yake ya kuingia Ikulu kama Rais aliyokuwa nayo toka mwaka 2005 na alishindwa kuingia mwaka 2010 kwa kumheshimu Rais Dr Kikwete pekee ila sasa ni zamu yake .
Pia alisema CCM bado ina nguvu zaidi katika jimbo la Iringa mjini na Tanzania kwa ujumla na iwapo suala la upendo likawatangulia watia nia wote pale wanapokosa kuteuliwa kuungana kwa upendo kumuunga mkono aliyeteuliwa kamwe suala la wapinzani kushinda litabaki kuwa ni ndoto.
Wakati huo huo huo mgombea huyo amewaacha hoi wanahabari waliofika kumsikiliza baada ya kudai kuwa waandike majina yao kamili na namba zao za simu ili kuja kuwakumbuka katika ufalme wake pindi atakapoingia Ikulu
|
Hakuna maoni
Chapisha Maoni