HABARI KUBWA LEO.PINDA,PROF-MUHONGO WAMECHAFUKA NA HAWASAFISHIKI URAIS CCM,SOMA HAPO KUJUA
Waziri mkuu Mizengo Pinda akichukua Fomu za Urais ndani ya Chama cha mapinduzi CCM leo mjini Dodoma |
ANAYEJIITA mtoto wa Mkulima Waziri mkuu Mizengo Pinda pamoja na Aliyekuwa Waziri wa Nisharti na Madini Sospeter Muhongo ambao wote kwa pamoja wamejitosa kwenye kivumbi cha Urais ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM,imeelezwa ni wachafu na hawasafishiki,Mtandao huu unaripoti Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Makada hao ambao walikuwepo kwenye Utawala unaomalizika wa Rais Jakaya kikwete wametajwa kuhusika kwa kiasi kikubwa katika kupotosha watanzania kwenye Mikataba mbali mbali nchini ambayo imekuwa mzigo kwa Watanzania.
Mizengo pinda, ambaye amechukua leo fomu ya Urais ndani ya CCM kwa stairi yake ya 'kimya kimya' huku akijatamba kukuza uchumi na kumalizia pale atakapoacha Rais Kikwete,anatajwa kukiweka wakati mgumu chama chake endapo kitampitisha kuwa mgombea wa Urais.
Pinda ambaye alijitwisha jukumu la kutetea ukwapuaji wa mabilioni ya Shilingi kwenye akaunt ya Tegeta Escrow iliyokuwa BOT na kudai fedha hizo kuwa sio "mali za Umma"
Mbali na hayo pia Pinda anatuhumiwa kuzembea,kunyamazia au kushindwa kuchukua hatua kwa Watendaji wake ambao waliruhusu pesa hizo bila kumalizika Kesi mahakamani. jambo ambalo lilimweka Bungeni kuwa miongoni mwa Vigogo waliotakiwa Kujiuzulu au kufukuzwa.
Jina la Pinda liliondolewa dakika za mwisho kwenye Orodha ya watuhumiwa Katika Kashfa ya Escrow baada ya "genge" la wabunge wa CCM kujiapiza kutounga mkono maazimio ya Bunge iwapo pinda kama atatakiwa kujiuzulu.
Duru zinasema Apizo la wabunge hao lilikuwa linaficha ukweli wa nani anahusika kushotwa kwa mabilioni ya Shilingi kupitia muamala wa Benki ya Stabinc,ambapo Vigogo wengie wa Ikulu wanatajwa kuwepo.
Sanjari na Ufisadi wa Escrow pia Waziri Mkuu Pinda anatuhumiwa katika ugawaji wa kiholela wa Vibali vya Sukari ambayo inadaiwa "Rushwa iliyokithiri katika kashfa ya Vibali vya Sukari"
Kada Mwigine wa chama hicho ambaye amejitosa naye anatajwa kwamba asafishiki ni Sospeter muhongo ambaye alijuzulu nafasi yake ya Uwaziri wa Nisharti na Madini baada ya kutuhumiwa kuhusika kama Dalali katika Kashfa ya Uchotwaji wa pesa za Esrow.
Muhongo ambaye aliruhusu pesa hizo kutoka huku wakati mashauri kati ya pande mbili kati ya Tanesco iko nchini ya Wizara ya Nisharti na madini na wabia wa kampuni ya IPTL amabo ni Bwana Seth na Rugemalira wakiwa bado hawajamalizana bado.
"Hawa watu wa CCM ni watu wa ajabu sana jamani huyo Muhongo akimbilia Urais kuficha madudu yake wakati sakata la Wizi wa Esrow bado ni kidonda kwa wananchi,leo anataka urais gani huu"amesema Mwananchi mmoja wa Mbezi aliyejitambulisha kwa jina la Jack.
Profesa Muhongo alijuzulu nafasi hiyo kwa madaha uku akijiinasibu kwamba yeye alipata malezi bora kwa wazazi wake.
Mbali na Esrow pia mhungo atuhumiwa kwa kushindwa kusimamia nafasi yake tangu mwaka 2012 alipochaguliwa kwa kitendo chake cha kuwakumbatia wawekezaji wa Kigeni na kushindwa kuweka mikataba ya madini hadharani,na kujunja katiba ya Jamhuri wa Muungano Ibara 63 (3) (a).
Muhongo pia amehusika akiwatusi wawekezaji wazawa akiwaita wanapesa za kuwekeza kwenye viwanda vya "Juisi na machungwa" huku akishindwa kuweka hoja madhubuti.
kwa mujibu wa Mtoa taarifa wetu aliyoko ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM ameupasha mtandao huu akisema Chama kinawakati mgumu sana kwani hakuna mgombea msafi.
"Sikiliza bwana sahivi CCM kinawakati mgumu sana wagombea wengi wamechafuka kwenye kashfa mbali mbali tena wengine wamejigeuza "UKAWA" kuishambulia Serikali ya Kikwete kama haijafanya kitu wakati wengi walikuwepo kwenye Utawala huo ambao Ufisadi,Rushwa,umasikini kukithiri pamoja na Suala la ajira kuwa kubwa"
Hakuna maoni
Chapisha Maoni