Zinazobamba

KUMEKUCHA SASA-WAISLAM WAJILIPUA SASA,WAMTANGAZIA KIAMA KIKWETE NA SERIKALI YAKE,MZIMU WA SHEHE PONDA WAIBUKA SOMA HAPA KUJUA

Pichani ni Mwenyekiti Jumuiya ya Taasis ya Kiislam
Sheikh Mussa Kundesha
Akizungumza na Wanahabari
leo Jijini dar es Salaa
awapo  Pichani

JUMUIYA na Taasis ya Kiislma nchini (T) imempa siku 15 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu,kuwaachia mara moja Viongozi wa Dini ya Kiislam waliokamatwa kama makosa mbali mbali la Sivyo Jumuiya hiyo itaitisha maandamano nchi nzima kupinga wanachodai ni uonevu wanaonewa na Serikali.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
         Kauli hiyo imetolewa Leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya  hiyo ambayo ni muunganiko wa Taasisi 11 za dini ya kiislam nchini Sheikh Mussa Kundesha Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amesema  Wameshoka na kile wanachodai ni kuonewa na Jeshi la Polisi kitendo cha kuvamia Misikiti mbali mbali nchini na kuwabambikizia Mashehe Kesi za Ugaidi na kushindwa kuwapa Dhamana.
         “Tumempa siku 15,mkuu wa Jeshi la Polisi nchini awe amewaanchi mara moja  viongozi wetu wa dini yetu waliokamatwa kwa kesi zisizo kuwa na kichwa na miguu,lasivyo akikaidi tutaitisha maandamo ya Amani kupinga uonevu huu”amesema Sheikh Kundesha.
      Shekh Kundesha ameongeza kuwa  mbali na Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi hao ,Lakini jeshi hilo limeshindwa kuwaachia kwa Dhamana viongozi hao, wakati huo huo amesema Jeshi hilo likiwaachia kwa Dhamana Maaskofu wanaotoa lugha za kichochezi ikiwamo Askofu Josephat Gwajima.
      “Huu ni uonevu gani tunafanyiwa na Serikali kwani Sheikh Ponda kwa sasa ni miaka miwili yupo ndani sio kwasababu ya Amri ya Mahakama bali ni ya Amri ya muendesha Mashtaka DPP eti kwa kutoa maneno ya kichochezi lakini kesi hiyo hiyo anayesema ni ya Uchochezi inaendana na Askofu Gwajima pamoja Viongozi wengine wa Dini ya Kikristo ,lakini wako huru vipi Shehe Ponda”Amehoji Sheikh Kundesha.
      Aidha,Sheikh Kundesha huku akiongea kwa Uchungu amesema kwa sasa Jumuiya hiyo imesikitishwa na kitendo anachokiita ni cha kuizika Dini ya Kiislam nchini kwa Jeshi la Polisi kuendeleza kuwakamata Walimu wanaofundisha watoto wa Dini ya hiyo kwenye Madrasa na kuwapa kesi mbali mbali.
       “Kule moshi mkoani Kilimanjaro watoto na Walimu wa Madrasa wamekamatwa kama ilivyokuwa Mkoani Mtwala Mwalimu wa  Madrasa  bado wanashikiliwa na Polisi kwa kuwa na watoto wanawafundisha Dini ya Kiislam “
      “Dodoma watoto wa tatu wa madrasa,Walimu wao na mwenye Nyumba wanakowafundisha watoto dini ya Kiislam waliwakamata na kupelekwa kituo cha polisi kuhojiwa na kuchukuliwa kama wahalifu wengine hivi nia ya serikali ni ipi”ameendelea kuhoji.
     Pamoja na hayo amebainisha kuwa kwa sasa Walimu ambao walikuwa wanafundisha madrasa wametangaza kuachana na kazi hiyo ya kuwapa Elimu watoto wa Kiislam kwa kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwapa kesi ya mbalimbali,

       Vilevile Sheikh huyo awataka waislam kujitokeza mnamo tarehe 15/05/2015 kwenye Maandamano hayo ya Amani kwa lengo la kupaza Sauti zao ili Dunia isikia mateso wanayoyapata Waislam wenzao nchini. 

No comments