HABARI KUBWA LEO-UKAWA WALISHUKIA GAZETI LA MTANZANIA,WASEMA WAPO GADO,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
| Pichani ni Viongozi wa UKAWA |
VIONGOZI wa Vyama Vikuu vya Upinzani vinavyounda (UKAWA)
Vimekanusha Uvumi unaoenezwa na Vyombo vya Habari kuwa Miongoni mwa Chama cha
siasa kinachounda umoja huo ambacho ni NCCR Mageuzi kwamba kimetoa hoja ya kujitoa kwenye umoja
Huo, na kusema huo ni upotoshaji Wa
Vyombo vya Habari ambavyo vinatumiwa na Chama cha Mapinduzi CCM.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kauli hiyo ya (UKAWA) inakuja ikiwa ,Gazeti
la moja linalotoka kila siku Gazeti la Mtanzania toreo la leo Tarehe 29-mwezi
wa nne mwaka huu bila ya kutaja chanzo cha uhakika kimeripoti Habari kwamba
Vyama hivyo vikuu vya Upinzania vimeshindwa kufikia muhafaka kwenye ugawaji wa
Majimbo na kudai kwamba Chama cha NCCR
mageuzi kimepeleka hoja ya kujitoa kwenye Umoja huo.
Wakikanusha taarifa hizo leo ,wakati
wakizungumza na Mtadao huu kwa Nyakati
Tofauti viongozi wa Ukawa unaoundwa na
Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD wameonyesha kusikitishwa na Taarifa
wanaodai ni ya kuzushi na zenye uwongo na kushangaa kuripotiwa kwenye Gazeti
ambalo wanasema limejaa wahariri mahiri nchini.
Wa kwaza kukanusha Taarifa hiyo ni
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dokta Wilboard Slaa ambapo amesema taarifa hizo zinalengo la kuwavunja
nguvu Watanzania kulekea kipindi hiki anachodai wanakwenda kushika Dola.
“Nashangaa sana hicho kigazeti
kuandika Taarifa ya uzushi kama hiyo,wakati ukweli ni kwamba kwa sasa tumefikia
asilimia 84 ya makubaliano ambayo tunakwenda vizuri sana na tena tupo kamili kuhakikisha
tunautoa utawala huu mbuvu wa CCM,leo anakuja mtu kwa kutumiwa huko anakuja na
taarifa za uongo kama hizo”Amesema Dokta Slaa.
Dokta Slaa ameongeza kuwa hata Hoja
ambayo wanasema kwa Chama mwenza wa Ukawa ambao ni NCCR Mageuzi kutoridhika na
Ugawaji wa Majimbo ya Ubunge kwenye Uchaguzi wa hapo baadae na kusema kwamba
wala kwenye Kikao kilichofanyika jana Jijini hapa ambacho pia leo kinaendelea,
wala hakijavunjika na wala chama cha NCCR hawajasema wataka kujitoa.
“Kwanza kikao cha Jana tulichokutana
na Viongozi wenzetu wa Ukawa hakijavunjika kama wanavyodai kwani hiyo hoja ya
Ugawaji wa Majimbo hatujazungumzia kwenye kiako hicho,kwani siku nzima
tulizungumzia namna ya kupata vyanzo vya pesa ili tuweze kufanya Kampeni nchi
nzima sasa huyo mwandishi wa Habari katoa wapi Taarifa hizo”ameendelea kusema
Dokta Slaa.
Mwandishi
wa Mtandao huu alipumuuliza ni Majimbo gani ambayo wanashindwa kufikiana,Dokta
Slaa amesema hawezi kujibu swali hilo kwani hayo ni mambo ya ndani ya Umoja huo
na akawataka Watanzania kuwa na subira wakati viongozi hao wakiweka mambo sawa
na kudai UKAWA watatoa wagombea Bora ambao anazidi dai watahakikisha wanaitoa
CCM Madarakani.
Kwa upande wake Mbunge wa Kigoma Kusin David
Kafulila ambaye pia ni Mjumbe wa kamati kuu ya NCCR-Mageuzi naye amekanusha
taaria hizo kwamba Chama hicho kimepeleka hoja za kujitoa kwenye UKAWA.
“Kiukweli
mimi nashangaa taarifa za upotoshaji kwenye Gazeti kama hilo,wakati ukweli ni
kwamba UKAWA tumefikia asilimia 84 ya makubaliano na wenzetu,eti leo tujitoe,maana sisi
tutakuwa watu wa ajabu sana ukweli ni kwamba hatujawai peleka hoja hizo na
vilevile,tupo kwenye asilimia za mwisho”amesema Kafulila.
Mbunge Kafulila amebanisha kuwa kwa
sasa umoja huo unaweka mipango ambayo anasema ni mizuri ya kuhakikisha kushinda
kwa kishindo kwenye uchaguzi Mkuu hapo baadae na kuwataka Watanzania kupuuza
Taarifa ambazo anaziita ni za kizushi.
Naye Kiongozi Mmoja wa Juu wa Chama
cha Wananchi CUF aliyezungumza na Mtandao
kwa sharti la kutotaja jina lake kwenye mtandao huu ambapo amfichua siri ambayo
anasema kwa sasa Chama cha Mapinduzi CCM
kimepeleka Fungu la pesa kwa waandishi wa Habari pamoja na Wahariri kuandika
Habari za upotoshaji juu ya UKAWA ili kuwapa hofu wananchi na hata alipoiona
Taarifa hiyo kwenye Gazeti la Mtanzania amedai kuwa hakuweza shangaa.
No comments
Post a Comment